'Nakupenda mama,'Yvette Obura amwambia Diana Marua baada ya kumtakia heri njema ya kuzaliwa

Muhtasari
  • Baada ya Yvette kuona ujumbe wake Diana alimjibu na kumwambia kwamba anampenda
Yvette Obura na Diana Marua
Yvette Obura na Diana Marua
Image: INSTAGRAM

Msanii iana B almaarufu Diana Marua kupitia kwenye ukurasa wake wa instagram alimtakia baby mama wa Bahati Yvette Obura heri njema anaposherehekea siku yake ya uzaliwa.

Diana aliahidi kumnunulia keki na kinywaji siku hii yake maalum.

Diana Marua na Yvette wameonyesha mfano mwema katika  kushiriki kumlea mtoto wao Mueni Bahati, kwani hawajakuwa na drama mitandaoni bali wamekuwa wakionyesha uhusiano mwema.

"Sheeeeeesssssshhh!!!! Mwangalieni😍👌 Happy Birthday Mama Mueni @yvette_obura champagne na birthday cake on me 🥂🍾Kwa miaka mingi zaidi ya Ajabu mbele❤️," Aliandika Diana Marua.

Baada ya Yvette kuona ujumbe wake Diana alimjibu na kumwambia kwamba anampenda.

"Awwwww thank you mama heav😍😍... unasema nigoje keki na champagne?I love you ma."