"Uliniacha pekee yangu, hukuwepo!" Zari amwambia Diamond sababu za kutengana naye

Muhtasari

• Zari amefunguka kuhusu sababu za kuchana na aliyekuwa mpenzi wake, Diamond Platnumz.

• Alisema Simba alimuacha mpweke bila wa kumkinga na kumtunza.

Zari Hassan na Diamond Platnumz
Zari Hassan na Diamond Platnumz
Image: INSTAGRAM// TIFFAH DANGOTE

Hatimaye mfanyibiashara na mwanasosholaiti, Zari amefunguka kuhusu chanzo cha ndoa yake na Diamond Platnumz kusambaratika.

Katika shoo ya Young,famous and African iliyopakiwa katika mtandao wa Netflix Ijumaa 18/3/2022, Zari alisema kwamba Simba alimuacha mpweke bila kujua nani wa kumkinga.

"...Ulikuwa wapi nilipokuhitaji? Uliniacha pekee yangu," Zari alisema.

Shoo hiyo ililenga kuelezea safari za maisha ya mastaa mbalimbali ambao wametusua katika maisha kwenye bara la Afrika.

Zari alikiri kwamba Diamond hakuwepo katika maisha yake wakati alikuwa akimhitaji zaidi, jambo ambalo lilimpelekea kufanya maamuzi mazito ya kutengana.

Akionekana kuwa mwenye machungu, Zari alisema kwamba ndoa yao ingekuwa imara iwapo Diamond Platnumz angetekeleza majukumu yake ipasavyo.

Diamond anasemekana kutokuwa mwaminifu katika mahusiano yao, jambo lililopelekea ndoa yao kusambaratika.