Nililipwa milioni 1 kunyoa 'dreadlocs' zangu-Thee Pluto afichua

Muhtasari
  • Thee Pluto afichua pesa alizolipwa ili kunyoa 'Dreadlocs' zake
Thee Pluto
Thee Pluto
Image: INSTAGRAM

Baada ya kuwa na dreadlocs kwa muda, na hata mashabiki kuzoea mtindo wake nywele Youtuber Thee Pluto ameamua kunyoa.

KIlichowashangaza wengi ni kuwa haukuwa uamuzi wake kunyoa bali ni rafiki ambaye alimthubutu anyoe.

Kupitia kwenye ukurasa wake rasmi wa Instagram, kwenye sekta ya Q&A aliwafiichulia mashabiki wake kwamba alilipwa milioni moja ili aweze kunyoa.

"Nini haswa kilichokusuma unyoe dreadlocs zako?"Mmoja wa mashabiki aliuliza.

Huku akijibu swali hilo alisema;

"Mambo kadhaa. Kubadilisha chapa, kutamani mabadiliko na muhimu zaidi nililipwa milioni 1 kutoka kwa rafiki baada ya kunithubutu,'' ilithibitisha Thee Pluto.

Thee Pluto ni mwanaYouTube wa Kenya ambaye amejitengenezea nafasi nzuri katika historia ya burudani ya Kenya kwa sehemu ya kipekee inayoitwa Jaribio la Uaminifu.

Pia alisema kwamba mara ya mwisho kumuona mwanawe iliwa miezi 6 iliyopita, kwani hakubalishwi kumuona.