Sababu ya kumuita mtoto wetu Mshindi-Evelyn Wanjiru afunguka

Muhtasari
  • Evelyn alibariikiwa na mtoto wake April 6 2022, huku akitoa sababu ya kumuita mwanawe kwa jina mshindi
Evelyn Wanjiru na mumewe
Evelyn Wanjiru na mumewe
Image: Instagram, KWA HISANI

Msanii wa nyimbo za injili Evelyn Wanjiru anasababu ya kutabasamu baada ya kubarikiwa na kifungua mimba, baada ya kusubiri kwa miaka 10.

Evelyn alibariikiwa na mtoto wake April 6 2022, huku akitoa sababu ya kumuita mwanawe kwa jina mshindi.

“Kabla baba hajafariki, tulikuwa tukizungumza na nikamuuliza, ‘Ikiwa tutapata mtoto, ungependa nimwite jina gani?’ Naye alizungumza moja kwa moja: Ikiwa ni mvulana, mwite. Mshindi. Nikamwambia, ‘Eh hilo jina linasikika kwa urahisi’ kwa sababu nilitaka majina haya kama Jayden! Hayo majina ya kisasa,

Ndipo tulipopata changamoto za miezi mitatu ya kwanza ambapo daktari alikuwa anatuambia mtoto anakuja na nikaanza kutangaza na kumwambia mtoto kuwa hatoki kabla ya muda wote wa ujauzito

Nilimkumbuka baba aliniambia kuhusu Mshindi. Unajua Mshindi ni mshindi. Mshindi. Umepigania ili uwe hapo ulipo. Kwa hiyo nilimpa mtoto jina hilo na tukaanza kumuita hivyo tangu wakati huo. Na unaona, ilidhihirika.”

“Nina furaha sana, nimesisimka na ninashukuru kwamba Mungu alitukumbuka katika mwaka wa kumi wa ndoa yetu,” alisema Evelyn.

Pia msanii huyo aliwashauri waunda maudhui kwamba wawache kuweka mambo yao hadharani sana, alisema haya huku akifichua sababu ya kutowaambia mashabiki wake kuhusu ujauzito wake.