Ninavyomlea isikusumbue-Nyota Ndogo alazimika kumtetea mwanawe mitandaoni

Asilimia kubwa ya mashabiki walimpongeza mwanawe Nyota kwa ujasiri wake wa kudensi.

Muhtasari
  • Shabiki huyo alikuwa anamkejeli mwanawe msanii huyo kwa mavazi yake, huku akimlaumu Nyota kwa malezi yake kwa mwanawe
Image: INSTAGRAM// NYOTA NDOGO

Msanii kutoka mkoa wa pwani Nyota Nogo, amelaziimika kumtetea mwanawe kutoka kwa shabiki ambaye aiamua kumkejeli.

Shabiki huyo alikuwa anamkejeli mwanawe msanii huyo kwa mavazi yake, huku akimlaumu Nyota kwa malezi yake kwa mwanawe.

Hii ni baada ya msanii Nyota kupakia video ya mwanawe akidensi, ili kupunguza mwili.

Nyota ni miongoni mwa wazazi ambao wamekuwa wakiwale awatoto wao peke yao,huku akionyesha mfano mwema kwa wazazi wengine kama yeye.

Kulingana na Nyota aliamka asubuhi na kumkosa mwanawe kitandani.

"Kuna maadili gani hapo ikiwa mzazi hana elimu ya malezi,"Shabiki alisema.

""Samahani sana, lakini kila mtu alee wake. Huyu ni wangu, navyomlea mimi isikusumbue wewe. Just lea wako vizuri na hiyo inatosha,"Alijinu Nyota Ndogo.

Asilimia kubwa ya mashabiki walimpongeza mwanawe Nyota kwa ujasiri wake wa kudensi.