Karen Nyamu ajibu kuhusu kuvunja ndoa ya Samidoh, video zao za uchi kusambazwa

Seneta Nyamu alibainisha kwamba hana mpango wa kuacha kumposti mwimbaji huyo.

Muhtasari

•Karen Nyamu amejipata akijibizana na wanamitandao ambao waliibua madai mazito dhidi ya mahusiano yake na Samidoh.

•Shabiki alidai kuwa hivi karibuni picha na video za uchi za seneta huyo na Samidoh zitavuma kwenye mitandao ya kijamii.

Samidoh na Karen Nyamu
Image: HISANI

Seneta wa kuteuliwa Karen Nyamu kwa mara nyingine amejipata pabaya na baadhi ya wafuatiliaji wake kwenye mtandao wa Instagram.

Katika siku chache zilizopita, mama huyo wa watoto watatu amejipata akijibizana na watumizi wa Instagram ambao waliibua madai mazito dhidi ya mahusiano yake na mwimbaji wa Mugithi Samuel Muchoki almaarufu Samidoh.

Chini ya chapisho lake la  siku ya Jumanne ambapo alipakia picha yake akiwa amevalia mavazi ya ufundi na kuandika  "Kujenga taifa, kihalisi", shabiki mmoja aliimshtumu kwa kuvunja ndoa ya Samidoh na Bi Edday Nderitu.

"Kujenga taifa na kuvunja ndoa ya mwanamke mwingine, wow tu wow! Nilijifunza katika shule ya msingi kuhusu  "Sifa za kiongozi bora" ,na unakosa baadhi ya sifa muhimu madam," janet.janto alimjibu seneta huyo.

Katika jibu lake, Nyamu alisema "Hiyo inaonekana kama shida yako mpendwa."

Katika chapisho lingine, shabiki alidai kuwa hivi karibuni picha na video za uchi za seneta huyo na Samidoh zitavuma kwenye mitandao ya kijamii baada ya video yao wakifurahia muda pamoja kusambaa mitandaoni hivi majuzi.

"Hizo video Zako unapost Kile tunangojea Ni mkiwa uchi Sasa. Naona umechizi😂... Kwanini ulete nyakati zako za siri na baba wa mtoto wako hadharani? Kama kulazimisha masuala ni mtu..," mwanamitandao alimwambia.

Huku akimjibu shabiki huyo, seneta Nyamu alibainisha kwamba hana mpango wa kuacha kumposti mwimbaji huyo.

"Nitamposti. Hicho kitabu ya viongozi unasoma choma," alijibu.

Mapema wiki hii, Video ya Nyamu na Samidoh wakifurahia wakati pamoja ilisambaa kwenye mitandao na kuzua hisia mseto miongoni mwa Wakenya ambao wamekuwa wakifuatilia hadithi yao ya mapenzi kwa karibu.

Katika video hiyo, Samidoh ambaye ni mwimbaji maarufu wa nyimbo za Mugithi alionekana na kusikika akimuimbia mama huyo wa watoto wake wawili wimbo wa injili wa Kikuyu huku wakiwa wamekaa kwenye kiti kimoja.

"Muiritu uyu, (Njeri) wuiguaga atia, wee utaigite murigo thii?

Njiguaga oo gugufuata wee utaigite murigo thii,

Njiguaga oo gugufuata tondu nduigite murigo thii,

Njiguaga oo njuke uhe,tondu nduigite murigo thii, " Samidoh aliimba huku akiwa amemlalia seneta huyo kwenye kifua.

Kumaanisha: "Msichana huyu (Njeri), huwa unajiskia vipi, kama bado hujaweka mzigo chini? Nahisi kukufuata kama bado hujaweka mzigo chini, huwa nahisi nikuje unipee kwa sababu hujaweka mzigo chini."

Wakati akimwimbia mzazi huyo mwenzake, Samidoh alionekana akimgusa kwenye kiuno na makalio kuashiria kile alichokuwa akiimba kuhusu.

Wakati huo, seneta Nyamu hakuweza kuficha furaha yake kubwa na alitabasamu wakati wote alipokuwa akirekodi tukio hilo la kupendeza. Nyamu hata alijiunga na staa huyo wa Mugithi katika kuimba wimbo huo.