Zari Hassan amsherehekea aliyekuwa mumewe, marehemu Ivan Ssemwanga kwa njia maalum

Zari alisherehekea urithi mkubwa ulioachwa na marehemu mfanyibiashara huyo na akadhihirisha kuendelea kwake.

Muhtasari

• Zari Hassan alichukua muda kumkumbuka baba huyo wa watoto wake watatu wakubwa na kumsherehekea 

•Bw Ssemwanga ambaye alifariki Mei 2017 angetimiza umri wa miaka 46 mnamo Desemba 12 waka huu kwani ilikuwa siku yake ya kuzaliwa.

amemsherekea marehemu mumewe.
Zari Hassan amemsherekea marehemu mumewe.
Image: HISANI

Siku ya Jumanne, mwanasholaiti maarufu wa Uganda na mfanyabiashara Zari Hassan alimsherehekea marehemu mumewe Ivan Ssemwanga kwa njia ya kipekee mnamo ambayo ilikuwa siku yake maalum.

Bw Ssemwanga ambaye alifariki Mei 2017 angetimiza umri wa miaka 46 mnamo Desemba 12 waka huu kwani ilikuwa siku yake ya kuzaliwa.

Licha ya yeye kuaga takriban miaka sita iliyopita, Zari Hassan alichukua muda kumkumbuka baba huyo wa watoto wake watatu wakubwa na kumsherehekea kwenye mitandao ya kijamii.

"Kheri ya siku ya kuzaliwa. Natumai malaika wanamsherehekea pamoja naye,” Zari aliandika kwenye picha ya marehemu bwenyenye huyo wa Uganda na mfanyibiashara aliyoichapisha kwenye Instagram.

Katika chapisho lingine, mama huyo wa watoto watano alishiriki picha ya kumbukumbu yake na marehemu mumewe wakistarehe kwa pamoja katika eneo la burudani..

Katika sehemu ya maelezo, alisherehekea urithi mkubwa ulioachwa na marehemu mfanyibiashara huyo na akahakikishia kuendelea kwake.

"Urithi unaendelea. Heri ya kuzaliwa," aliandika.

Mwanasholaiti huyo mrembo na marehemu Ssemwanga walikuwa kwa ndoa rasmi kwa takriban miaka miwili kabla ya kutengana mwaka 2013. Waganda hao wawili waliokuwa wakiishi na kufanya kazi Afrika Kusini walikuwa na watoto watatu pamoja.

Bw Ssemwanga, ambaye alikuwa mfanyibiashara tajika nchini Afrika Kusini alifariki katika hospitali ya Steve Biko Academic, jijini Pretoria, Afrika Kusini ambako alikuwa amekimbizwa akiwa katika hali mbaya.

Baadaye alizikwa kijijini kwao Nakaliro katika hafla ghali iliyohudhuriwa na watu maarufu na matajiri nchini Uganda na kwingineko ikiwa ni pamoja na wanamuziki Jose Chameleone, Bobi Wine, SK Mbuga na Weasel.

Kiasi kikubwa cha pesa na mvinyo ghali vilimwagwa ndani ya kaburi la mfanyibiashara huyo baada ya jeneza lake kuteremshwa. 

Ssemwanga ambaye alitambulika kama kiongozi wa Rich Gang nchini Uganda alifariki akiwa na umri wa miaka 39 na aliacha nyuma watoto watatu wa kiume ambao alikuwa amepata na mwanasoshalaiti Zari Hassan.

Wawili hao walikuwa kwenye ndoa kwa zaidi ya mwongo mmoja na kujaliwa watoto watatu pamoja kabla ya kutengana. Baadae Zari alijitosa kwenye mahusiano na Diamond na kupata watoto wengine wawili naye.