Zuchu ampiga busu zito Diamond baada ya kumsherehekea kwa mfululizo wa maua kuelekea kitandani (+video)

Zuchu alifurahishwa sana na kitendo cha Diamond na kumpiga busu zuri mdomoni baada ya kupanda kitandani.

Muhtasari

•Bosi huyo wa WCB alitumia fursa hiyo kueleza kwa ubunifu mapenzi yake kwa malkia huyo kutoka Zanzibar ambaye pia anadaiwa kuwa mpenzi wake.

•Diamond alionekana kuzidiwa na hisia baada ya kufungua zawadi hiyo ya gharama kubwa ambayo aliambiwa imetoka kwa mpenzi wake.

alofurahi baada ya Diamond kumsurprise
Zuchu alofurahi baada ya Diamond kumsurprise
Image: INSTAGRAM// WASAFI TV

Staa wa Bongo fleva, Naseeb Abdul Juma almaarufu Diamond Platnumz mnamo siku ya Jumatano alimfanyia suprise kubwa na ya kupendeza msanii wake Zuhura Othman, maarufu kwa jina la Zuchu.

Ikiwa ni siku ya wapendanao, bosi huyo wa WCB alitumia fursa hiyo kueleza kwa ubunifu mapenzi yake kwa malkia huyo kutoka Zanzibar ambaye pia anadaiwa kuwa mpenzi wake.

Video iliyoshirikiwa na Wasafi Media inaonyesha Diamond akimuongoza malkia huyu wake kwenye chumba kilichojaa maua mekundu, puto na mapambo mengine ya kupendeza. Chumba hicho kilijazwa na mada ya upendo na njia ya maua haikuongoza mahali pengine isipokuwa chumba cha kulala.

"Wow, hii ni nzuri. Hii ni nzuri. Naipenda,” Zuchu aliyekuwa amevalia nguo za njano alisema huku akifuata mkondo wa maua.

Kwenye kuta za chumba cha kulala kulikuwa na puto maridadi zilizopangwa vizuri ili kutengeneza maneno “Happy Valentines Zuuh.”

“Hii ni nzuri. Asante,” Zuchu alimwambia Diamond huku akisogea kumbusu kwenye midomo.

Hapo awali, malkia huyo wa WCB alikuwa amemzawadia bosi huyo wake simu ya bei ghali sana ya iPhone 15 ili kumsherehekea mnamo siku ya wapendanao.

Diamond alionekana kuzidiwa na hisia za furaha baada ya kufungua zawadi hiyo ya gharama kubwa ambayo aliambiwa imetoka kwa mpenzi wake.

Wiki kadhaa zilizopita, Diamond Platnumz aliwakanganya mashabiki wake kuhusu uhusiano wake na Zuchu baada ya kutangaza waziwazi kwamba yuko single kisha akabadilisha kauli yake muda mfupi baadaye.

Staa huyo wa bongo alitangaza kuwa sasa hayupo kwenye mahusiano yoyote, na kuzua mjadala mkubwa kwenye mitandao ya kijamii.

“Kuanzia leo na kuendelea ningependa niwatangaze rasmi kuwa I AM SINGLE, sidate wala sina mahusiano na mwanamke yeyote," Diamond alisema katika taarifa yake ya katikati mwa Januari.

Aliendelea kuwaomba mashabiki wakome kumhusisha na mwanamke yeyote akiahidi kutangaza hadharani mwenyewe pindi atakapopata tena mapenzi.

"Hivyo nisiwekewe mwanamke yeyote kama mwanamke wangu, itakapotokea kudate ama kuwa na mahusiano nitawajuza ama kutambulisha kama jinsi huwa nafanya kila wakati," alisema.

Tangazo hilo ambalo alitoa kwenye Instastori zake lilizua mjadala mkubwa kwenye mitandao ya kijamii huku wengi wakihisi amemalizana na Zuchu.

 Hata hivyo, mnamo saa chache baadaye, staa huyo wa Bongo alitoa taarifa nyingine akitangaza kwamba hawezi kuvumilia maisha ya ukapera.

"Niwajulishe tu kwamba swala la usingle limeshindikana hivyo naendelea kula raha Hubani kwenye kisiwa na kitongoji kilekile cha karafuu," Simba alitangaza.

Aidha, aliwadhihaki na kuwatupia vijembe watu waliotarajia mwisho wa uhusiano wake akisema kwamba watu huwa hawaachani tu hivyohivyo.

“Wote mliokuwa mnashadadia poleni sana, siku nyingine acheni papara, mjifunze kusikiliza ata kidogo! Watu hawaachani kifala tu hivyo,” alisema.