Rafiki wa Jowie avunja kimya baada ya kuhukumiwa kwa rafiki yake

Akitoa uamuzi huo Jumatano, Jaji wa Mahakama Kuu Grace Nzioka alisema mauaji ya kutisha ya Monica Kimani yalikuwa ya "kusudi."

Muhtasari
  • kwa alichokipost, ilionekana rafiki yake Jowie alificha ukweli na alikuwa akimlinda mtu ambaye labda alihusika na uhalifu.
Jowie na Hamez Githinji
Image: Instagram

Rafiki wa Joseph Irungu "Jowie", Hamez Githinji kama anavyojiita Instagram,  alishtua mashabiki  kwa alichochapisha katika instastories zake .

kwa alichokipost, ilionekana rafiki yake Jowie alificha ukweli na alikuwa akimlinda mtu ambaye labda alihusika na uhalifu.

"Iligharimu kiasi gani kubeba msalaba wa mtu kaburini kwako?? Walikuahidi watakutoa?? kiri ukweli jamani!!

Pia alimhakikishia jowie kwamba anaweza kuomba tena hukumu hiyo.

"Unaweza kuomba tena hukumu hiyo... Tafadhali iambie dunia ukweli... Unajua ni nani aliyefanya hivyo??...

Chapisho lake lilipata maoni tofauti tofauti  kutoka kwa Wakenya. Wengine waliamini kuwa Jowie hakutenda kosa, wengine wakidhani kuwa anaongea tu huku wengine wakiuliza kwanini ameamua kuongea sasa hivi kujaribu kumwokoa rafiki yake.

Mwezi uliopita Jowie alipatikana na hatia ya mauaji ya Monica Kimani, ambaye aliuawa kikatili katika nyumba yake ya Lamuria Gardens jijini Nairobi usiku wa Septemba 19, 2018.

Hakimu Nzioka aliamua kuwa upande wa mashtaka ulitoa ushahidi wa kutosha na kuthibitisha bila shaka kuwa Jowie kweli alimuua Monica.

Akitoa uamuzi huo Jumatano, Jaji wa Mahakama Kuu Grace Nzioka alisema mauaji ya kutisha ya Monica Kimani yalikuwa ya "kusudi."

"Mauaji yanaacha nyuma njia ya ndoto zilizovunjika na mioyo iliyovunjika ambayo haiwezi kuponywa."

"Kitendo cha mauaji ni uhalifu wa kutisha ambao unapinga muundo wa maadili wa jamii na unadai haki," Grace Nzioka alieleza mahakama.

Jowie hivi sasa amehukumiwa kifo baada ya kupatikana na hatia ya mauaji ya mfanyabiashara Monica Kimani 2018.