Butita aomba wanamitandao kuacha kumhusisha na ‘story’ za Mammito

Butita kwa ucheshi alishiriki video ya marehemu rais Mwai Kibaki na mkewe, Lucy Kibaki wakati wa mkutano na wanahabari.

Muhtasari
  • Baadhi ya maoni yalikuwa yakimtaja Butita na hii ndiyo sababu iliyomfanya atoe ufafanuzi kwa wanamtandao kuwa hana uhusiano wowote na Mammito.
Instagram, KWA HISANI
Instagram, KWA HISANI
Image: Eddie Butita

Mchekeshaji Edie Butita amewataka Wakenya kutomhusisha na masuala ya Mammito.

Butita kwa ucheshi alipakia video ya marehemu rais Mwai Kibaki na mkewe, Lucy Kibaki wakati wa mkutano na wanahabari.

Lucy alikuwa ameitisha mkutano wa waandishi wa habari kwa rais huyo wa zamani kutangaza kwamba alikuwa na mke mmoja tu.

"Kila mtu anajua kuwa nimeoa, na nina mke mmoja tu. Vyombo vya habari vinaendelea kurudia kwamba nina mke au wake mwingine, lakini nataka kuweka wazi kuwa nina mke mmoja tu na ni  Lucy."

Mchekeshaji huyo aliweka wazi kuwa hayuko kwenye uhusiano na mcheshi huyo na kunukuu kipande hicho:

"Ifahamike......... Wacheni kuniingiza kwa hii story."

Eunice Wanjiru almaaarufu Mammito hivi majuzi alikuwa ameingia kwenye vichwa vya habari baada ya kumkejeli Jowie Irungu kwa video ambayo ilisambaa mitandaoni na kuvuma kwenye X.

Baadhi ya wananchi walimsapoti huku wengine hawakuona video yake ya kuchekesha hata kidogo.

Baadhi ya maoni yalikuwa yakimtaja Butita na hii ndiyo sababu iliyomfanya atoe ufafanuzi kwa wanamtandao kuwa hana uhusiano wowote na Mammito.