Oga obinna na YY wanazozana juu ya upendeleo wa wake wa "Kienyeji"

Mnamo Machi 20, Oga obinna alishiriki video akiwashauri watu binafsi kuzingatia kuoa wanawake kutoka maeneo ya mashambani badala ya kutoka mijini.

Muhtasari
  • Obinna, akihisi kukerwa na pingamizi za YY, aliingia kwenye mitandao ya kijamii kwa mara nyingine tena kupinga msimamo wa YY.
YY na Oga Obinna
Image: Hisani

Malumbano yamezuka kati ya Oga Obinna na mcheshi YY baada ya kutoa maoni kinzani kuhusu mada ya wife material.

Mnamo Machi 20, Oga obinna alipakia video akiwashauri watu binafsi kuzingatia kuoa wanawake kutoka maeneo ya mashambani badala ya kutoka mijini.

Alisisitiza umuhimu wa kutafuta wanawake ambao hawajaonyeshwa sana mitandao ya kijamii na maisha ya jiji, akipendekeza kwamba anaweza kushauri kuhusu sifa zinazohitajika zaidi kwa ndoa.

"Sai vile vitu zinaenda, kama unataka kuoa inabidii uende ushago huko ndani. Si zile ushago ziko kwa vituo vya soko. Utafute kienyeji mwingine mwenye hajui mtandao wa kijamii na hajui Obinna ni nani. Yaani hajui nini inafanyika wapi. Lakini ni kitu moja safi, alafu sasa unaanza kumchanua polepole lakini ukisema unataka kuoa Nairobi ama Kisumu ama Mombasa kitakuramba", Obinna alisema.

Kujibu madai ya Obinna, YY alisema kuwa kusafisha ndio sehemu mbaya zaidi. Alitaja wanawake huwa na tabia ya kuwazidi wenzi wao wanapoendelea kimaisha, mara nyingi huwa wanasahau waliowaunga mkono njiani.

Aliongeza kuwa anahitaji juhudi za ziada kwa mwanamke kuendelea kujituma baada ya kupata mafanikio.

"Hiyo kusafisha ndio mbaya zaidi.....Sio asili yao kukauka pale wanapoogea.... mwanamke anapokua na wewe bado ni mtu yule yule uwe unaendelea vizuri wanaamini wamekuzidi...."

"Siku zote wanataka juu zaidi ili wakipanda ngazi, wanachukulia ardhi kuwa sawa.....wengi hawatakumbuka waliowaweka hapo. Inamhitaji mwanamke juhudi za ziada dhidi ya asili yake kuishi nawe baada ya kufanya hayo yote....na wanawake hao ni nadra", YY alisema.

Obinna, akihisi kukerwa na kanusho la YY, aliingia kwenye mitandao ya kijamii kwa mara nyingine tena kupinga msimamo wa YY.

Alimhoji YY kwa kukosoa maoni yake kuhusu kuchagua mke, akionyesha kwamba YY mwenyewe alikuwa amechagua kuoa mwanamke ambaye huenda "alimsafisha".

Kwa hivyo nilizungumza kuhusu kusafisha mwanamke na YY anasema hiyo ni mbaya.......oooh ukimsafisha utakuja akuwache sijui nini.....lakini subiri kidog, YY si umesafisha bibi yako? 

"Jinsi anavyoonekana sasa si kama alivyoonekana ulipomtambulisha kwetu kwa mara ya kwanza. Kwa nini unahubiri divai na wewe mwenyewe unakunya maji ? Sisi hatutaki tutafute watu tusafishe?" Alisema.

Kwa kujibu shutuma za Obinna, YY alifafanua kauli yake ya awali, akimtaka Obinna kuwakilisha kwa usahihi maoni yake.

Alimtaka Obinna kurejea maoni yake na kushughulikia moja kwa moja, badala ya kuyatafsiri vibaya kwa ajili ya mabishano.

"Soma maoni yangu tena na nukuu ni kama nilivyosema.....Si kama ulivyoitafsiri.....naona hata umeunda sauti kutokana na nilichoandika......rudi nyuma, soma na ufanye video inayosema nilichosema kabisa....... Kisha tunaweza kuwa na mjadala huu", YY aliandika.