Mchungaji Kanyari amsihi Nyako amruhusu kutumia TikTok kwa amani

Kanyari aliomba ruhusa mama huyo wa watoto watatu na akalijitolea kumwombea.

Muhtasari
  • Ombi lake lilikuja siku chache baada ya Nyako kuwakosoa wachungaji kama James Ng'ang'a, Kanyari na wengine kwa kujiunga na jukwaa hilo.
Kanyari na Nyako
Image: Hisani

Mhubiri maarufu  wa Kenya Victor Kanyari amemsihi mwanatiktok Nyako amruhusu kutumia mtandao huo kwa amani siku chache baada ya kujiunga na mtandao wa kijamii.

Ombi lake lilikuja siku chache baada ya aliyejitangaza kuwa rais wa TikTok nchini Kenya Nyako, kuwakosoa wachungaji kama James Ng'ang'a, Kanyari na wengine kwa kujiunga na jukwaa hilo la kijamii.  

Nyako alidai wengi watafunga makanisa hivi karibuni  kwa sababu vijana walikuwa hawaendi tena kwenye maeneo ya ibada.

Hata hivyo, alipokuwa katika kipindi cha moja kwa moja, Kanyari alijitolea kumwombea mama huyo wa watoto watatu ambaye siku za nyuma aliwahi kutabiriwa na mtu mwingine wa Mungu kuhusu kifo chake.

"Ni kwa sababu sijui. Unajua anaweza kuitwa Nyako kwenye TikTok lakini ana jina tofauti kama Wairimu au Waitherera. Sijui, laiti ningemjua Nyako ni nani, laiti ningemjua huyo mwanamke. sijui anapoishi au yuko wapi. Naomba nikuombee kwa jina la Mungu , na unikaribishe hapa kwenye TikTok, na Mungu atakubariki," Kanyari alisema.

Mara baada ya kumaliza kuongelesha Nyako, Kanyari aliomba watu wamtumie zawadi, na mtu mmoja akamtumia pesa {money gun}, ambayo ilimfanya aruke huku akiweka pozi la saini ya Christiano Ronaldo.

Tazama baadhi ya maoni kutoka kwa watumiaji wa mtandao kuhusu video iliyo hapo juu;

wilby: Not kanyari minding her own business 😂😂😂 ata asomi comments

DEE EBBA 💕💕: who told him when he comes to TikTok he should say tap tap your screen 😂

Catherine: Ofcourse he will pray for nyako🤣🤣🤣🤣

wangeci_Ngugi: 🤣🤣🤣I'm loving this

♥️Śôṉîâ’ś Kïṉg❤️: ATI I'm a new year 😂😂😂

Eric followed you 🇰🇪🇺🇬🇹🇿: Kanyari will be a news make here😂😂Wacha ashike line

Akolo Faith: sasa Nani anamwambia moneygun ni 150k pale comment section 😂😂😂