Nilitaka kuwa mhubiri nikiwa katika Chuo Kikuu- mbunge Peter Salasya

Mbunge huyo mcheshi alifichua kwamba mojawapo ya matamanio yake bora ilikuwa kukuwa mhubiri.

Muhtasari
  • “Baada ya chuo kikuu, nilifundisha chuoni, nikipata mshahara mdogo wa Shilingi 10,000 kwa mwezi. Wakati fulani, mambo yalipoenda vizuri, ningeweza kupata Shilingi 13,000,”
MBUNGE PETER SALASYA
Image: HISANI

Peter Kalerwa Salasya, Mbunge wa Mumias Mashariki, anayejulikana  kama PK Salasya, hivi majuzi alizungumzia matarajio yake alipokuwa katika chuo kikuu.

Mbunge huyo mcheshi alifichua kwamba mojawapo ya matamanio yake bora ilikuwa kukuwa  mhubiri.

Alifichua hayo wakati akitoa hotuba ya umma katika Chuo Kikuu cha Pwani katika Kaunti ya Kilifi, hafla ambayo ilihudhuriwa na Naibu Rais Rigathi Gachagua.

Bw Salasya, mhitimu wa Chuo Kikuu cha Egerton, alisimulia tukio la wakati alipokuwa chuo kikuu mwaka wa 2011.

“Nilipojiunga na Chuo Kikuu cha Egerton mnamo 2011, mhadhiri alitumia saa moja kuzungumza na wanafunzi wa mwaka wa kwanza kuhusu matamanio yao. Ilipofika zamu yangu, nilisema nataka kuwa mchungaji au kiongozi. Kila mtu aliangua kicheko,” Salasya alisema kwa kicheko.

Salasya, mbunge wa muhula wa kwanza aliyechaguliwa mwaka wa 2022 chini ya chama cha Democratic Action Party - Kenya (DAP-K), alisisitiza azma yake ya kutekeleza azma yake ya kisiasa licha ya kufikiria kazi ya kuhubiri awali.

“Baada ya chuo kikuu, nilifundisha chuoni, nikipata mshahara mdogo wa Shilingi 10,000 kwa mwezi. Wakati fulani, mambo yalipoenda vizuri, ningeweza kupata Shilingi 13,000,” alisema.

Lakini mapenzi yake yalibaki kwenye siasa.

"Mnamo 2022, niliamua kujaribu siasa na nikafanikiwa kugombea nafasi ya mbunge," Salasya alisema, akiwahimiza wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Pwani kutekeleza ndoto na matamanio yao kwa moyo wote.

Mbunge huyo, ni mtumiaji  wa mtandaoni ambaye hupeleka ucheshi wake kwenye tovuti za mitandao ya kijamii.

Wabunge wengine ambao walihudhuria hafla katika Chuo Kikuu cha Pwani ni; Owen Baya (Mbunge wa Kilifi Kaskazini), John Methu (Seneta wa Nyandarua), Gitonga Mukunji (Mbunge wa Manyatta), Eric Wamumbi (Mbunge wa Mathira), Njeri Maina (Mwakilishi wa Wanawake wa Kirinyaga), Kuria Kimani ( Mbunge wa Molo), Stanley Muthama (Mbunge wa Lamu Magharibi), Joseph Githuku (Seneta, Kaunti ya Lamu), Josses Lelmengit (Mbunge wa Emgwen) na Charles Kanyi (Mbunge wa Zamani wa Starehe na Cate Waruguru (Aliyekuwa Mwakilishi wa Wanawake wa Laikipia), miongoni mwa wengine.