Stephen Letoo aeleza kwa nini yeye na mkewe wataenda sehemu tofauti kwa honeymoon

Letoo alipendekeza wazo jipya; kila mmmoja wao angechagua eneo tofauti la kwenda honeymoon pekee yao.

Muhtasari
  • Letoo alionyesha nia yake ya kumwacha bibi harusi wake aamue anakotaka kwenda, huku yeye pia akichagua anakoenda.
STEPHEN LETOO
STEPHEN LETOO
Image: Facebook

Mwanahabari wa runinga ya Citizen Stephen Letoo amewaacha mashabiki wakishangazwa na mbinu yake isiyo ya kawaida ya mipango ya honeymoon, akitangaza kuwa yeye na mchumba wake hawatakuwa na honeymoon ya kawaida baada ya harusi pamoja.

Katika mahojiano na Oga Obinna, alielezea mtazamo wake kuhusu mipango ya honeymoon, akisema kuwa sio kawaida yao kufuata njia ya kawaida ya kwenda mahali sawa na mke wake.

Badala yake, Letoo alipendekeza wazo jipya;  kila mmmoja wao angechagua eneo tofauti la kwenda honeymoon pekee yao.

Letoo alionyesha nia yake ya kumwacha bibi harusi wake aamue anakotaka kwenda, huku yeye pia akichagua anakoenda.

Alisisitiza kuwa sababu ya honeymoon ni kustarehe  baada ya uchovu wa kupanga harusi, badala ya kuhisi shinikizo la kupata mtoto nje ya nchi.

"Nilimwambia mgeni mkuu wa hiyo siku achague ni wapi anataka kwenda. Mimi Nitaenda honeymoon yangu mwenyewe na yeye ataenda yake. Honeymoon inapaswa kuwa ya kufuta jasho ambalo umepata kupitia mipango madhubuti sana.Siyo kwenda kusumbuana kutafuta mtoto ughaibuni," Letoo alieleza.

Aliangazia nia yake ya kuchagua anakoenda kulingana na matakwa ya kibinafsi, iwe ni makazi tulivu ya Maasai Mara au burudani huko Dubai.

Vivyo hivyo, alionyesha kuunga mkono uamuzi wa mke wake, hata ikiwa ataamua kusafiri na marafiki kwenda mahali tofauti

"Mimi ntachagua yangu kama ntaenda Masaai Mara ntaenda na yeye atachagua hata kama ni dubai ataenda na marafiki zake," Letoo alisema