Maoni mseto baada wanawake wawili wa Tanzania kusema Kenya haina wanawake warembo

Kwa mujibu wa wawili hao, Watanzania walistahili kushika nafasi ya kwanza kwa kuwa wanawake wote katika nchi hiyo inayoongozwa na Samia Suluhu ni warembo.

Muhtasari
  • Katika ripoti hiyo, wanawake wa Ethiopia walishika nafasi ya kwanza, Wanigeria wakashika nafasi ya pili kisha Watanzania kisha Wakenya na Waafrika Kusini katika nafasi za nne na tano mtawalia.
Wanawake wawili kutoka Tanzania waliosema hawajaiona wanawake warembo kutoka Keya
Image: Instagram

Wanawake wawili wa Tanzania wameibua hasira kwa kijamii ya watumiaji wa mitandao baada ya kusema kuwa hakuna wanawake warembo nchini Kenya.

Wakijibu ripoti iliyowaorodhesha wanawake wa Kenya kama wanawake wa nne warembo barani Afrika, wanawake hao wawili walisema nafasi waliyopewa wanawake wa Kenya hawakustahili kupewa.

Katika ripoti hiyo, wanawake wa Ethiopia walishika nafasi ya kwanza, Wanigeria wakashika nafasi ya pili kisha Watanzania kisha Wakenya na Waafrika Kusini katika nafasi za nne na tano mtawalia.

Kwa mujibu wa wawili hao, Watanzania walistahili kushika nafasi ya kwanza kwa kuwa wanawake wote katika nchi hiyo inayoongozwa na Samia Suluhu ni warembo.

"Kenya hakuna wanawake warembo. Umewaona? Labda ni kwa sababu sijafika Kenya, lakini Watanzania walistahili nafasi ya kwanza. Wanawake wote hapa Tanzania ni warembo", alisema mwanamke mmoja.

Wakenya kwenye mitandao ya kijamii waliwajibu wawili hao kwa kuwatusi wanawake wenzao kwa ushupavu.

Haya hapa ni baadhi ya maoni kutoka kwa watumiaji wa mtandao;

mwaliko8: Vipi dada unatafuta ugonvi😒😒😍

irenerito wazza:  Huyu naye ni nani? Na anaenda wapiπŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚

k.michaellah: Tanzanians believe being light skinned is beautyπŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚lLord have mercy

omarrijal: All black women are beautiful and I respect that much blessings

carol Keithia: Anataka atrend KenyaπŸ˜‚πŸ˜‚..Ng'ooo ..Tuko busy na mafuriko.

kabeeria_atheru: Kupaka mkorogo sio uremboπŸ˜‚

Rukia 231: Nguvu ya kuonyesha sura natural hamna mumejiza makeup tele juu ya mkorogo kisha mwajiona muwarembo....toeni makeup muongee vizuri

Ruth Rosah: They should say whatever they are saying in English.

Maswai Chelagat: They have already started a battle.

Emmie Moseri:  I am more beautiful than those women speaking. I come in peace.