Harmonize na mzazi mwenzake Shanteel wamsherehekea binti yao akitimiza miaka 6

Zuuh ni mtoto wa pekee wa Harmonize aliyempata wakati wa mahusiano mafupi na mfanyibiashara Official Shanteel.

Muhtasari

•Zulekha anaadhimisha siku yake ya kuzaliwa ya 6 leo, Mei 30, na wazazi hao wamechapisha posti maalum za kumsherehekea.

•Kwa upande wake, Bi Shanteel alimtakia binti yao siku njema ya kuzaliwa na kusherehekea ukuaji wake.

Image: INSTAGRAM// HARMONIZE

Staa wa Bongo, Rajab Abdul Kahali almaarufu Harmonize pamoja na mzazi mwenzake Official Shanteel wamemsherehekea binti yao Zulekha Rajabu almaarufu Zuuh Konde kwenye siku yake ya kuzaliwa.

Msichana huyo mrembo anaadhimisha siku yake ya kuzaliwa ya sita hivi leo, Mei 30, na wazazi hao wawili wamechapisha posti maalum za kumsherehekea.

Konde Boy alichapisha picha nzuri za bintiye kwenye ukurasa wake wa Instagram na kuelezea  jinsi anavyojivunia msichana huyo mdogo.

“Nimebahatika kuwa baba yako,” Harmonize alisema.

Kwa upande wake, Bi Shanteel alimtakia binti yao siku njema ya kuzaliwa na kusherehekea ukuaji wake.

Pia alitumia fursa hiyo kufunguka kuhusu baraka na furaha nyingi ambazo msichana huyo amemletea maishani mwake.

“Kheri ya siku ya kuzaliwa binti yangu mzuri, Mungu ni mwema na mwingi wa baraka, ni mwaka mwingine tena tukiwa na furaha na Amani, umekuwa mtoto mwenye baraka umeleta Nuru na furaha maishani mwangu,Nakupenda sana sana binti yangu @zuuh_konde,” Shanteel alisema.

Zuuh Konde ni mtoto wa pekee wa Harmonize ambaye alimpata wakati wa mahusiano mafupi na mfanyibiashara Official Shanteel.

Official Shanteel alikuwa na uhusiano wa kimapenzi na Harmonize wakati mwanamuziki huyo alikuwa bado akichumbiana na Sarah Michelloti. Uhusiano huo wa kipindi kifupi ulifanya wawili hao kujaliwa mtoto mmoja  wa kike pamoja, Zulekha Nasra (Zuuh Konde) na pia ulivunja ndoa ya bosi huyo wa Kondegang na Sarah.

Mwaka wa 2021, Harmonize alipokuwa akizindua albamu yake  'High School' alifunguka kuhusu utata uliozingira kuzaliwa kwa bintiye.

Mwimbaji huyo alifichua kwamba kuzaliwa kwa mtoto huyo ndicho chanzo cha kuvunjika kwa ndoa yake ya kwanza na Sarah Michelloti.

Harmonize alisema ndoa yao ya miaka minne ilianza kusambaratika wakati mpenzi wake alikuwa amesafiri kuenda kwao na baada ya kuwa pweke kwa muda akapata majaribu ya kutembea na mwanadada aliyemzalia mtoto.

"Ilikuja kipindi akawa anasafiri kuenda kwao. Nilikuwa Tanzania na kama unavyojua umbali wa mapenzi unapokuwa nikaishia kutembea na mwanamke ni mama Zuuh sasa hivi. Kwa mipango ya mwenyezi Mungu nikamfanya mjamzito." Harmonize alisema.

Konde Boy alifichua kwamba Shanteel alikuwa na wasiwasi kuhusu ujauzito huo na hata alikuwa tayari kuutoa ila akamkataza.

Alisema kuwa alikubali majukumu na akahudumia ujauzito ujauzito hadi mtoto alipozaliwa