Kama singetoroka, ningeishia kuwa mtumizi wa mihadarati- Akothee afunguka alivyogura ndoa yake

"Kama singetoroka, ningeishia kuwa mtumizi wa dawa za kulevya ili kupunguza maumivu," alisema.

Muhtasari

•Takriban mwongo mmoja uliopita, Akothee alikuwa kwenye ndoa na mzungu ambaye alipata naye mtoto mmoja wa kiume.

•Alisema licha ya kuhuzunika kwa jinsi alivyomuacha mumewe, ilimbidi awaokoe watoto wake kutokana na fedheha ya mara kwa mara.

Akothee
Akothee
Image: HISANI

Mwanamuziki na mjasiriamali mashuhuri wa Kenya Esther Akoth almaarufu Akothee amefunguka kuhusu jinsi alivyogura ndoa yake na baba wa mtoto wake wa mwisho.

Takriban mwongo mmoja uliopita, mama huyo wa watoto watano alikuwa kwenye ndoa na mzungu ambaye alipata naye mtoto mmoja wa kiume. Wenzi hao walikuwa wakiishi jijini Mombasa pamoja na watoto wengine wa mwimbaji huyo.

Msanii huyo mwenye umri wa miaka 43 amemtaja mume huyo wake wa zamani kama mpenzi sumu na kusema kwamba alilazimika kukimbia ndoa hiyo kwa sababu ikiwa angekosa, basi angeweza kuishia kutumia dawa za kulevya.

"Hii ilikuwa kabla ya wanablogu kuwa na wivu. Na kisha baada ya kufikiria sana, niligundua kuwa sasa ningeweza kusimama kwa miguu yangu kifedha na ningeweza kuwapa watoto wangu kilicho bora zaidi. Kwanza nilienda Nairobi, nikajipatia nyumba nzuri, nikainunulia samani, na kupata msaidizi wa nyumba. Nilimfunza msaidizi wa nyumbani kwa miezi 3. Kisha nikapeleka wavulana shule ya Braeuburn. Ilikuwa rahisi kwa sababu nilihitaji tu kuwahamisha kutoka Braeuban Mombasa hadi Nairobi. Nilihamisha biashara zangu pia,” Akothee alisimulia.

wakati alipogura ndoa yake takriban mwongo mmoja uliopita.
Picha za maktaba za Akothee na watoto wake wakati alipogura ndoa yake takriban mwongo mmoja uliopita.
Image: FACEBOOK// AKOTHEE

Mama huyo wa watoto watano alifichua kuwa alichukua hatua hiyo ya kutoroka baada ya kurejea nchini kutoka Afrika Kusini alikokuwa amekwenda kurekodi video ya muziki na Diamond Platnumz.

“Sikuhitaji kubeba chochote kutoka nyumbani. Kwa hivyo, ningeweza tu kuja nyumbani kama mtu asiye na hatia kama mwanamke aliye tayari kutulia. Nilipuuza kelele zote. Kwa kweli, siku ya mwisho, tulikunywa glasi ya divai pamoja, jaduong iliniruhusu kuwapeleka watoto shuleni asubuhi iliyofuata. Na hivyo ndivyo tulivyoendesha moja kwa moja hadi uwanja wa ndege. Wasichana walikuwa na memo ya sisi kutoroka asubuhi kwanza ilibidi wavae Dera ili kuchanganya mazingira yote, wavulana hawakuwa na habari ya kile kilichokuwa kikiendelea. Kwao ni shule kama kawaida na mama anawaacha.  Hadi tunapita shule yao walianza kuuliza maswali 🤔,” alisema.

Akothee alidokeza kuwa licha ya kuhuzunika kwa jinsi alivyomuacha mzazi mwenzake, ilimbidi kuwaokoa watoto wake kutokana na fedheha ya mara kwa mara.

"Kama singeondoka, ningeishia kuwa mtumizi wa dawa za kulevya ili kupunguza maumivu," alisema.

Alidokeza kuwa kuhama kwake kulikuja na matatizo fulani kwani wazazi wenzake sasa walitaka kuwatembelea watoto wao katika nyumba yake mpya jijini Nairobi.