Karen Nyamu amtaka Ruto kuwachukulia hatua maafisa waliowauwa waandamanaji wasio na hatia

Nyamu alisisitiza kuwa utovu wa nidhamu na utovu wa baadhi ya maafisa wa polisi umekuwa ukiharibu imani na usalama wa wananchi.

Muhtasari
  • Nyamu, ambaye amekuwa akizungumzia masuala mbalimbali yanayohusu nchi aliitaka serikali kuwachukulia hatua maafisa waliowaua waandamanaji jana.
KAREN NYAMU
KAREN NYAMU
Image: HISANI

Seneta mteule Karen Nyamu amekashifu maafisa wa polisi wanaodaiwa kuwapiga risasi na kuwaua waandamanaji nje ya majengo ya Bunge.

Nyamu, ambaye amekuwa akizungumzia masuala mbalimbali yanayohusu nchi aliitaka serikali kuwachukulia hatua maafisa waliowaua waandamanaji jana.

"Kwa nini kupiga risasi kuua?? kwa nini kuwafyatulia risasi waandamanaji wasio na silaha? Eleza! je, bunge ni muhimu zaidi kuliko maisha ya watoto wetu? Walitaka tu kusikilizwa," Karen aliandika kwenye ukurasa wake wa Instagram.

"Rais William Samoei Ruto, ni wakati sasa wa kuwachukulia hatua wale maafisa wasio na taaluma walioua waandamanaji! Wanachafua utawala wako kwa njia mbaya zaidi! Unaongeza mapato tu, hatuko vitani!!"

Nyamu alisisitiza kuwa utovu wa nidhamu na utovu wa baadhi ya maafisa wa polisi umekuwa ukiharibu imani na usalama wa wananchi.

Aliomba uchunguzi wa kina ufanyike kuhusu tuhuma za utovu wa nidhamu wa polisi na kutekelezwa kwa hatua kali za kuhakikisha uwajibikaji.

Jana polisi walionekana wakiwafyatulia risasi waandamanaji ovyo na bado waandamanaji walikuwa na sauti na simu zao tu ambazo walizitumia kueleza matatizo yao.

Kwa sasa watu kadhaa wanahofiwa kufariki huku wengine wakiuguza majeraha yao katika hospitali kote nchini.