Mume wangu halipi kodi ya nyumba ilhali nikilipa anawaleta wanawake-Mwanamke asimulia

Muhtasari
  • Mwanamke asimulia masaibu ambayo amekuwa akipitia mikononi mwa mumewe
  • Mwanamke huyo alisema kwamba amekuwa akimfanyia mumewe kila kitu lakini haoni hayo yote
sad woman
sad woman

Ni kitu kipi ambacho wanawake hawajapitia wakiwa mikononi mwa waume zao au wapenzi wao licha ya wao kuwapenda sana?

Mwanamke wa umri wa kati akisimulia masaibu ambayo amekuwa akipitia mikononi mwa mumewe kwa miaka mitatu sasa aliwaacha wengi wakishindwa ni upendo wa aina gani ambao anampenda mumewe.

Huu hapa usimulizi wa mwanamke huyo;

 

"Nimekuwa na mume wangu kwa miaka mitatu, nikimwambia alipe nyumba ananiambia kwamba atalipa siku yenye mwenye nyumba ataweka kufuli

Ninafanya kazi nalipa nyumba, namnunulia nguo,viatu na hata na nunua chakula, ndio mume wangu anafanya kazi lakini pesa zake ni za kubugia vileo, na kujivinjari

Nimejaribu kutoka kwake  mara nyingi sana lakini ananifuata na kuniomba msamaha kisha namsamehe kwa maana nina mpenda sana na moyo wangu wote." Alisimulia Mwanamke huyo.

Alizidi na usimulizi wake huku akifichua licha ya yake kulipa kodi ya nyumba mumewe amekuwa akiwaleta wanawake na kufanya ngono nao.

"Nikilipa kodi ya nyumba mume wangu huwa anawaleta wanawake kila siku na kufanya mapenzi na wao

Nikimuuliza ata nipa kichapo cha mbwa na kisha ananifungia nje, lakini licha ya hayo yote bado nampenda mume wangu na roho yangu yote kwa maana sijawahi ona mwanamume mwingine kama yeye." Aliogeza.