Lazima niwafanyie watoto wangu DNA wakizaliwa-Mwanamume akiri

Je ni yapi ambayo mume wako alifanya ama hufanya ili kuhakikisha uhusiano na ndoa yenu imedumu?

Si mmoja au wawili ambao hufanya jambo na kuwaacha wengi midomo wazi, pia kuna wale wataweka masharti katika boma yao ambayo yanapaswa kufuatwa kila siku.

Mwanamume mmoja aliwacha wengi na maswali mengi baada ya kufichua lazima wanawe wafanyiwe DNA ili kuhakikisha kwamba mtoto ni wake.

 

Huku akijitetea alisema kwamba anamuamini mkewe lakini hataki drama au kumlea mtoto na mwishowe baba yake anakuja na kusema huyyo mtoto ni wake baada ya kumlea katika maisha yake.

Haya yalijiri baada ya Mama Dangote kusema kwamba Mzee Abdul si baba yake staa wa bongo Diiamond Platnumz.

Ni jambo ambalo liliwashangaza mashabiki wengina kuachwa na maswali, lakini je mama huyo anatafuta kiki kulingana na mashabiki wengi?

Huu hapa usimulizi wa mwanamume huyo;

"Lazima niwafanyie watoto wangu DNA, ili kuhakikisha ni wangu, si ati simuamini mke wangu lakini nataka kuhakikisha hakutakuwa na drama yeyote maishani mwangu baada ya kuwalea watoto wangu

Sitaki mwanamume ajitokeze na kusema kuwa mtoto wangu ni wake." Alisimulia mwanamume huyo.