'Ninamchumba lakini si mheshimiwa,'Natalie Tewa aweka mambo wazi huku akisema hana chuki na Edgar Obare

Muhtasari
  • Natalie Tewa asema hana chuki na mwanablogu Edgar Obare
  • Pia alisema kwamba ana mchumba lakini si mwanasiasa
  • Tewa alidai kwamba si mjamzito kama vile madai yalikuwa yameenea
Natalie tewa
Natalie tewa

Youtuber Natalie Tewa kwa mara ya kwanza amezungumzia uhusiano wake wa kimapenzi na jinsi hana chuki na mwanablogu Edgar Obare.

Mwaka jana madai yalienea kwamba Tewa ni mpenzi wa mwanasiasa, ilhali hajawahi kuthibitisha wala kukana madai hayo.

Tewa hajakuwa kwenye mitandao ya kijamii kwa muda sasa,kupitia kwenye ukurasa wake wa instagram sekta ya maswali na majibu mmoja wa mashabiki wake alimuuliza kama ni mchumba wa mheshimiwa.

 

"Je wewe ni mchumba wa mheshimwa wetu." Shabiki aliuliza.

Natalie Tewa alikuwa na haya ya kumjibu

Oolisikia wapi." yaani ina maana kuwa yeey si mchumba wa mheshimiwa.

Mwingine alimuuliza kama anamchumba na akasema ndio.

Ugomvi kati ya mwanablogu Edgar Obare na Tewa  ulishuhudiwa sana na mashabiki huku mmoja wa mashabiki wake akimuuliza kuhusu Edgar Obare.

"Haumpendi Edgar Obare?" Natalie alimjibu 

"Mimi sina chuki."

Pia uvumi ulikuwa umeenea kwamba Natalie ana ujauzito ambapo alikana madai hayo.