Mpenzi wake muigizaji Baha azima uvumi kwamba ana ujauzito

Muhtasari
  • Mpenzi wake muigizaji Baha azima uvumi kwamba ana ujauzito
Baha na mpenzi wake Georgina Njenga
Image: Hisani

Mpenzi wa muigizaji wa zamani wa Machachari Baha, Georgine Njenga amepuuza vikali madai kwamba anatarajia mtoto wake wa kwanza na muigizaji huyo.

Georgina alishiriki  maoni ya wanamtandao kwenye chapisho lake la Instagram akidai wanaweza kusikia harufu ya ujauzito, ikifuatiwa na maelezo mafupi na wazi.

"Sina ujauzito," Georgina aliandika ujumbe wake.

Mapenzi ya wawili hao yamekuwa yakishuhudiwa na mashabiki mitandaoni kwani wamekuwa wakipakia picha zao huku wakifurahia wakati wao pamoja.

Muigizaji Baha ni miongoni mwa watu mashuhuri ambao waliamua kuanza mapenzi wakiwa na umri wa chini, huku wakiwa mfano mwema kwa vijana wengi mitandaoni.

Kwenye video hiyo, Georgina aliangazia njia kadhaa ambazo watu huelezea wengine kwa sababu tu ni wanene sana na alisema kuwani wakati kila mtu kuacha tabia hiyo kwa sababu inapunguza kujithamini.

Mashabiki waligundua kuwa Georgina alikuwa amebadilika na wakaanza kumpongeza wakidai wanaweza kuona ujauzito wake.