Je Diana Marua amefanya uamuzi bora kwa kujiunga na tasnia ya muziki?

Muhtasari
  • Mama huyo wa watoto wawili atatambulika kwa jina la kisanii, Diana_B, akijiita Queen of African Rap
Image: INSTAGRAM//DIANA MARUA

Diana Marua, mke wa mwimbaji Bahati amezindua kazi yake ya muziki.

Siku ya Jumapili, Bahati alifanya tafrija kubwa katika hoteli ya Trade Mark, ambapo Diana alitambulishwa kama msanii wa muziki.

Mama huyo wa watoto wawili atatambulika kwa jina la kisanii, Diana_B, akijiita Queen of African Rap.

Saa kadhaa baadaye, wimbo mpya wa Diana 'Hatutaachana' ulianza kuonyeshwa kwenye YouTube. Katika wimbo huo, Diana anazungumzia uhusiano wake na Bahati.

"Hii ni kubwa,  wacha hiyo ufala wa Eric Omondi, hii ni kubwa kwa Kenya," Mwimbaji Bahati alisema, kabla ya kumuingiza mkewe kwenye jukwaa.

Na hatimaye alipopanda jukwaani, aliwatumbuiza mashabiki wake kwa kibao chake.

"Wanaosema tutaachana, sidanganyi watangoja sana, yetu si ya konde boy na Kajala...mapenzi ya kujienjoy za kifala, ama kama Lilian. na gavana, vita vya Chris Brown na Rihanna... Bahati na Marua tamu kama halua..."

"Uko tayari?" 

Wageni wake walioalikwa kwenye uzinduzi huo ni pamoja na mwanamuziki Akothee, ambaye alimpigia debe Diana B kama "Rapper Mkubwa wa Kike Afrika"

"Iko wapi nduru ya msanii mkubwa Afrika nzima? Akothee alisema,"

"Je, mtu anaweza kunipatia taulo, ninatoka jasho, Ikiwa haujashtuka leo ... wangapi wameshtushwa na ufichuzi wa Bahati."

Katika maoni yako je Diana amefana uamuzi bora kwa kujiunga na tasnia hiyo? na ni yapi unatarajia kutoka kwake?