Makena Njeri asherehekea kuhitimu miaka 30 kwa ujumbe maalum

Makena Njeri
Image: Studio

Mkurugenzi Mtendaji na Mwanzilishi wa Bold Network Africa, Makena Njeri,Jumanne alitumia ukurusa wake wa Instagram kuadhimisha siku ya kuzaliwa.

Katika ujumbe wake, Makena aliangazia baadhi ya mambo ambayo amejifunza katika kipindi cha miongo mitatu ambacho kimepita. Makena Njeri alisherekea  kuhitimu miaka 30.

Alijivunia  miaka yake ya 20's kwa sababu ni katika kipindi hicho  ambapo alifika Nairobi.

Sikuwaza kamwe kwamba wakati fulani maishani ningefanya uamuzi wa kuruka na kuja katika jiji kubwa! Nairobi. Nilikuja hapa kwa sababu. Na ni miaka kumi tu baadaye ndipo ninaielewa zaidi! "Siku moja usiku unalala kwenye benchi kwenye mitaa katikati ya jiji kuu, miaka michache ijayo unakuwa mada inayovuma kila unapochagua kuzungumza na kuishi ukweli wako, msimu ujao unatafuta kusudi lako na kuanza tembea safari hiyo bila woga,” aliandika.

 Makena alieleza kuwa safari hiyo ijakuwa rahisi kwani ukakamavu wake na majaribu mengi lakini thawabu zimekuwa za jasho lake mwenyewe.

Nimekutana na roho za warembo katika jiji hili, nimependa sana jiji hili, nimepata familia na marafiki ambao wamenipenda na kuniweka juu bila kujali. Moyo wangu umejaa shukrani ninapoaga miaka yangu ya 20. Ninabeba masomo na kuendelea hadi 30 yangu kwa hekima zaidi. “Somo langu kubwa ninapotafakari miaka hiyo kumi. Haijalishi unafanya nini, unakutana na nani, wanakuambia nini, kamwe usisahau WEWE NI NANI!