Sio mimi,'Babu Owino akana madai ya kuwa mwanamume aliyeonekana akipigana kwenye tamasha ya Konshens

Muhtasari
  • Mwanasiasa huyo alisema kuwa Konshens alipokuwa akitumbuiza mashabika Carnivore, alikuwa akimtumbuiza mke wake
Mbunge wa Embakasi Mshariki Babu Owino
Image: Babu Owino/INSTAGRAM

Mbunge wa Embakasi Mashariki Babu Owino amekana kuwa mwanamume aliyeonekana kujihusisha katika ugomvi kwenye tamasha la Mwaka Mpya la Wimbi la NRG.

Tukio hilo lililofanyika Ijumaa, Desemba 31, lilikuwa maarufu kwa sababu msanii kutoka Jamaica Konshens alikuwa akiwatumbuiza mashabiki, lakini inaonekana baadhi ya matukio yalifanyika nyuma, ambayo wengi hawakuyafahamu.

Mwanasiasa huyo alisema kuwa Konshens alipokuwa akitumbuiza mashabika Carnivore, alikuwa akimtumbuiza mke wake.

Maelezo yake yalisomeka;

"Kwa heshima, sikuwa kwenye sherehe ya Konshens, na mtu anayedaiwa kuwa mimi kwenye video inayoenea mitandaoni sio mimi. Wakati Konshens alikuwa akiwatumbuiza mashabiki wake pia nilikuwa nikitumbuiza  mke wangu na anaweza kushuhudia. Watu kwenye karamu ya Konshen pia wanapaswa kuthibitisha kwamba sikuwapo,"Babu aisema.