Miracle Baby awajibu wanaouliza Sailors walizama wapi

Muhtasari

•Baadhi ya mambo aliyotaja kama chanzo cha kukosa kutoa wimbo mpya msimu  huu wa sherehe ni kwamba, akaunti zao zilitolewa pesa, mikataba ya mamilioni ya pesa ilipigwa vita na watu ambao hakuwataja 

Sailors-3-551x600
Sailors-3-551x600
Image: Hisani

Mwanamuziki wa Gengetone, Miracle Baby amefunguka na kueleza kilichosababisha kikundi cha  Sailors kukawia bila kutoa muziki 

 Miracle Baby ambaye ni mmoja wa  kikundi cha Sailors, ambacho kinajumuisha wasanii wengine kama Shalqido, Lexxy Yunng, Masilver na Oogosjuma amepuuzilia mbali kwamba wamekosana huku akieleza changamoto zilizowakumba.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram, Miracle Baby aliulizwa swali na shabiki, mbona kikundi hicho kimekawia sana bila kutoa wimbo mpya wa burudani kama mbeleni.  Kwa kauli iliyovutia macho wengi, mwanamuziki huyo alijibu kwa maneno yaliyoashiria machungu aliyonayo,

 "Na hii swali ya kijinga mtu asiwai niuliza tena  ..."Alisema Miracle Baby huku akiendelea kusema, kila mtu anajua kilichosababisha utepetevu wa  kikundi hicho chao.

Baadhi ya mambo aliyotaja kama chanzo cha kukosa kutoa wimbo mpya msimu  huu wa sherehe ni kwamba, akaunti zao zilitolewa pesa, mikataba ya mamilioni ya pesa ilipigwa vita na watu ambao hakuwataja 

"Dunia mzima ilikuwa, na ikaona tukinyanganywa vitu zetu zote, ikiwemo na akaunti zetu, pesa zetu, mikataba ya mamilioni ikapingwa na mnajua ni akina nani walifanya hivo... lakini ikanyamaziwa" alidokeza 

Aliendelea kuwaeleza mashabiki wake kuwa kwa sasa anashughulika na jambo ambalo litamletea chakula kwa meza mambo mengine hataki kusikia.

"Sioni tukisaidiana na maswali za kijinga  nkt!!! ndio maana nafanya chenye kitaniletea chakula kwa meza"