'Asante kwa kuniruhusu kuwa mmoja wenu,'Kambua awashukuru mashabiki

Muhtasari
  • Isitoshe, aliwashukuru wote waliofanikisha safari yake ikiwemo na Kampuni ya Royal Media ambayo ilimpa nafasi ya  kuendeleza injili
mwanamuziki wa injili Kambua
mwanamuziki wa injili Kambua
Image: instagram/ Kambua

Msanii wa nyimbo za  injili  Kambua hatimaye amejitokeza na kuwashukuru mashabiki wake kwa kuweza kuwa naye wakati wa kipindi chake.

Mwimbaji huyo ambaye alihudumu katika runinga  moja nchini. amechapisha taarifa kupitia ukurasa wake wa instagram, akionekana kama alihisi kuwa wakati wake, kwenye kipindi hicho ulikuwa umefika tamati hii ni  baada ya  kuhudumia  jumuiya  ya Kikristu kwa takribani miaka 12. 

"Nimekua, nimejifunza, na kupenda kuwa sehemu ya maisha yenu,kuja kwenye vyumba vyenu vya kuishi kila Jumapili asubuhi," alisema Kambua.

Isitoshe, aliwashukuru wote waliofanikisha safari yake ikiwemo na Kampuni ya Royal Media ambayo ilimpa nafasi ya  kuendeleza injili.

Asante! Kwa huduma za Royal Media, wafanyakazi wenzangu wote wa ajabu, familia yangu na marafiki, asante kwa kuniruhusu kuwa mmoja wenyu,asante kwa  yote ambayo Mungu aliniumba niwe, bila kizuizi. Ninaweza kutazamia chochote ambacho kitanijia wakati ujao, kwa sababu imani." alisema Kambua