Ningekutungia wimbo,'Mcheshi YY amwambia mpenzi wake baada ya kujifungua

Muhtasari
  • Hata hivyo alimwambia achague mahali ambapo anahitaji kuenda ili ampeleke kama njia ya kumpongeza

Mcheshi maarufu nchini YY kupitia kwenye ukurasa wake wa instagram alitangaza kwamba amebarikiwa na kifungua mimba msichana.

Habarii hizo zilikuwa za kushangaza kwa wengi wa mashabiki wake, kwani mchekeshaji huyo hajawahi mpakia mpenzi wake mitandaoni.

YY pia alimshukuru mpenzi wake kwa kumpa zawadi ya kipekee, huku akisema kwamba angemtungia wimbo.

Hata hivyo alimwambia achague mahali ambapo anahitaji kuenda ili ampeleke kama njia ya kumpongeza.

"Mama kwa binti wa Mfalme❤...nguvu kuliko Moissanite...ningekutungia wimbo lakini umeshika gitaa langu mkononi...siwezi kukuambia vya kutosha jinsi ninavyoheshimu kujitolea kwako. ...Asante kwa kusukuma....Nataka uchague sehemu ambayo ungependa kutembelea..na isikuwe nje ya Nairobi tafadhali ni January🤪🙏," YY Aliandika.

Mashabiki walichukua fursa hiyo na kumpongeza mchekeshaji huyo na mpenzi wake.