Hana kitu,'Mpenziwe Stivo Simple Boy amwaya mtama'

Muhtasari
  • Mpenziwe Stivo Simple Boy afichua wanayoyafanya usimamizi wake

Mpenzi wa Stivo Simple Boy Pritty amezua taharuki mtandaoni, baada ya kufichua ukweli kuhusu jinsi mameneja wa Stivo Simple Boy unavyomnyanyasa.

Akiongea kwenye mahojiano, Pritty alisema kuwa Stivo hana pesa licha ya kushiriki na kufanya kazi na lebo kadhaa.

Alisema kuwa usimamizi wake ukiongozwa na Oyoo, wanakula pesa ambazo Stivo hulipwa kila mara na chapa.

Akiongea na mwanablogu wa Kenya  alisema;

"Kila kitu ambacho umesikia kuhusu usimamizi ni kweli, Simple Boy hawezi kufanya lolote, nami pia siwezi. Ataendelea kufanya kile anachopenda. mpaka Mungu atakapomfungulia njia nyingine ambapo anaweza kufanya vizuri zaidi na kuwa mahali ambapo ana furaha."

Lakini Pritty alisema, “Kama sasa hivi, uongozi haunipendi, sijui wamefanya nini, haruhusiwi kuja kuniona.

Pritty alidai kuwa Stivo alitumbuiza katika Maisha Magic East, na akalipwa shilingi 120,000, lakini uongozi ulimlipa 4000pekee. Huwa wanachukua zaidi ya robo tatu ya mshahara wa Stivo.

"Ninahisi kama wanamdhibiti na kwamba wakati fulani hunifanya nijisikie kukosa nguvu. Anadhibitiwa na usimamizi wake, kwa sasa hatuwasiliani baada ya TikTok yangu kusambaa mitandaoni."

Aliongeza, "Uongozi hauongei na mimi, wiki iliyopita Instagram yangu iliripotiwa sikuweza kupost chochote kwa hiyo sijui ni nani aliyefanya hivyo lakini aliyefanya anataka kuniangusha."

Swali kuu ni je nani anasema ukweli kati na usimamizi wake msanii huyo,mpenziwe na msanii Stivo.