Diamond na Zuchu ni wapenzi – Juma Lokole atoboa

Muhtasari

• Hivi majuzi Zuchu alijitokeza hadharani na kushukuru mpenzi wake ambaye jina lake alilibana kwa kumnunulia mdoli mkubwa. 

• Juma, amebaini kuwa Diamond na Zuchu wamekuwa kwenye mahusiano kwa takribani mwezi mmoja.

 

Diamond na Zuchu
Diamond na Zuchu
Image: hisani

Baada ya tetesi kuibuka kwamba mwanamuziki nguli Diamond platnumz anacheza unyumba  na Moja wa wasanii wake, Zuchu.

Ni bayana kuwa wanamuziki hao wako katika mahusiano, kupitia taarifa ya mtangazaji wa Wasafi Fm na mwandani wa Diamond,Juma Lokole.

Juma, amebaini kuwa Diamond na Zuchu wamekuwa kwenye mahusiano kwa takribani mwezi mmoja.

“unajua ukweli mapenzi hayafichiki na ni vizuri tuweke mambo wazi…Zuchu na Diamond wana mahusiano...Hivi sasa ni mwezi mmoja ”.. alisema Juma lokole.

Vile vile walijaribu kumpigia simu Diamond ilikuthibitisha habari hizo ambapo alikataa kuchukua simu yake huku akiwandikia arafa kwamba amesikia wanachotaka kumuliza.

Hivi majuzi Zuchu alijitokeza hadharani na kushukuru mpenzi wake ambaye jina lake alilibana kwa kumnunulia mdoli mkubwa Ikumbukwe Mwezi uliopita, Diamond na Zuchu walionekana pamoja.

Tangu hapo mashabiki walianza madai wanalegezana nyoyo.