Zaa wako umfiche,'Vera Sidika amshambulia shabiki aliyemwambia awache kupakia mwanawe mitandaoni

Muhtasari
  • Vera Sidika amshambulia shabiki aliyemwambia awache kupakia mwanawe mitandaoni
Image: INSTAGRAM// VERA SIDIKA

Kufuatia madai ya Huddah yawatu mashuhuri washerehekea kupata mimba kwa umaarufu na kutumia watoto wao kwa umaarufu,hatimaye Vera Sidika amevinja kimya.

Huddah Monroe, mwenye ushawishi mkubwa mitandaoni alitumia mitandao yake ya instagram kuwashutumu wanawake ambao hutumia mimba kwa mwenendo na pia kutumia watoto wao kujifanya kuwa maarufu.

Bila shaka, yote yalielekezewa Vera Sidika, ambaye amekuwa akiboresha mitandao ya kijamii na picha za binti yake mwenye umri wa miezi mitatu, Asia Brown.

Vera hakuwacha hayo yaende bure kwani aliwashauri wanamitandao wanaokejeli malezi yake waweze kuzaa watoto wao.

Mama huyo pia alifichua jinsi alimpa mmoja wa wafuasi wake block baada ya kumsuta jinsi amekuwa akimpakia mwanawe mitandaoni.

"Niletee huu ujinga na upate block!!! hakuna mbu yeyote ambaye ataniambia jinsi ya kumlea mtoto wangu ,nyinyi nyote hamkumbeba kwa miezi tisa ili mtoe maoni ya jinsi anavyolelewa Zaa wako ufiche! Pls Mind your uterus as I mind my own," Vera Aliandika.

Kulingana na wanamitandao maneno yake Vera yalikuwa yanamwendea Huddah, ambaye aliwakashifu watu mashuhuri kwa kuwapakia waoto wao mitandaoni.