Akuku Danger ana moyo wa dhahabu-Sandra Dacha asema huku akifichua uhusiano wake na mcheshi huyo

Muhtasari
  • Mwigizaji huyo pia alifichua muda ambao wamekuwa pamoja na sifa maalum zinazomfanya avutiwe na mchekeshaji huyo
Sandra Dacha
Image: Moses Mwangi

Muigiaji Sandra Dacha anayefahamika sana kama Silprosa kwa mara ya kwanza amewajibu mashabiki wake ambao wamekuwa wakiuliza uhusiano wake na mcheshi Akuku Danger.

Akiwa kwenye mahojiano na mpasho, wakati wa hafla ya kuchangisha pesa za kulipa bili ya mcheshi huyo alisema kwamba ana uhakika kwamba mpenzi wake atarudi nyumbani.

"Akuku is my Bae...he is my boyfriend. Now that he is healed, Kijana anafaa aende nyumbani, akule na akule ndio apone kabisa. Kijana saizi hakuli vizuri. If you gerrit you gerrit," Sandra Dacha alifichua.

Mwigizaji huyo pia alifichua muda ambao wamekuwa pamoja na sifa maalum zinazomfanya avutiwe na mchekeshaji huyo.

"Mwaka mmoja, unajua dawa ya puto ni sindano. Yeye ni aina yangu. Akuku ana moyo wa dhahabu...kisha tabasamu lake...oh Mungu wangu. Ni mtu mzuri," Sandra Dacha alisema.

Harambee iliyofanyika katika Ukumbi wa Kitaifa wa Kenya siku ya Alhamisi ilileta pamoja wacheshi, wasanii na waigizaji.

Katika kikao hicho, wasanii walifanikiwa kukusanya takriban 164,000 ambazo zitatumika kulipia kwa kiasi bili ya hospitali ya Ksh 1 Milioni.

Sandra alisema michango hiyo itaendelea hadi Akuku Danger atakapofanikiwa kurudi nyumbani.