Mambo ni shwari kati ya Rayvanny na mpenziwe Paula Kajala

Muhtasari

•Paula kajala ambaye ni mtoto wa muigizaji maarufu Tanzania Kajala Masanja.Wiki jana, wapenzi hao waliachana kufuatiliana kwenye ukurasa wao huku Paula akifuta picha alichokuwa amechapisha kwenye ukurusa  wake wa Instagram

•Ikumbukwe Baba Levo alijitokeza Jumanne na kueleza kwamba alimuonya Ravyaan kuhusu kulipia mpenzi wake karo,  akisema mpenzi hasomeshwi kwa sababu akipata elimu kukuzidi  atakutoroka.

Image: INSTAGRAM// RAYVANNY

 Baada ya staa wa Bongo flavor Raymond Mwakyusa almaarufu Rayvanny kuacha kufuata mpenzi wake Paula Kajala kwenye ukurusa wa Instagram, tetesi ziliibuka kwamba wapenzi hao wamechana.

Wiki jana Paula Kajala ambaye ni mtoto wa muigizaji maarufu Tanzania Kajala Masanja na Rayvanny waliacha kufuatana kwenye mtandao wa Instagram huku mlimbwende huyo  akifuta picha alizokuwa amepakia.

Sasa imebainika wawili hao wamerudi kufuatana  baada ya wiki moja ya tetesi kuwa wameachana kuenea mitandaoni.

Kulingana na  kitendo cha kurejea kufuatilia kwenye mitandao ni bayana wazi kuwa hali mambo yako shwari kati yao.

Ikumbukwe Baba Levo alijitokeza Jumanne na kueleza kwamba alimuonya Ravyaan kuhusu kulipia mpenzi wake karo,  akisema mpenzi hasomeshwi kwani akipata elimu kukuzidi  atakutoroka.

Haya yamejiri siku chache baada ya Fayvaan ambaye ni Baby mama wa Ravyaan kusema ikiwa mwanamitindo Kim Kardashian waliachana na Rapa wa Marekani Kanye West sembuse wao.

Alisema hayo wakati alipokuwa akijibu shabiki moja aliyemwambia  aliyemliza kwa nini huwa hataki kuacha Ravyaan.

Kinachusibiriwa  sasa nikuona  kama wapenzi hao watachapicha picha pamoja na kuandikiana jumbe tamu za mapenzi kama ilivyo ada yao.