Mpenzi mpya wa Zari? uvumi mitandaoni kuwa ashapata mshikaji

Zari na Gk Choppa
Zari na Gk Choppa
Image: instagram/zari

 Mwanasosholaiti na mfanyabiashara  sifika Zari the Boss Lady amejitokeza na kuzungumzia  mwanamume aliyeonekana naye kwenye picha moja ambayo imekuwa ikisambazwa  mitandaoni.

Kupitia  kituo kimoja cha habari cha  Uganda, ambacho kilimhoji Zari, alieleza kuwa jamaa aliyekuwa naye kwenye video  iliyosambazwa mitandaoni ni rafiki yake na si mpenzi wake kama wanamtandao wanavyodhani.

"ni rafiki yangu huyu,tafadhali  acheni kueneza uongo mtandaoni," alisema Zari.

Baada ya meza ya udaku kupiga mbizi ili kupata kina cha uvumi huu ilibainisha jina halisi la jamaa huyo kuwa  GK Choppa ambaye ni tajiri sifika Afrika Kusini.

Vilevile, Gk Choppa ameonekana kuchapisha  video iliyokuwa ikionyesha akimkaribisha  Zari kwenye himaya yake. 

Zari,ambaye ni mpenzi wa zamani wa Diamond Platinmuz na Mama wa watoto wawili wa msanii huyo, tangu waachane na Diamond hajakuwa  akiposti picha na wanaume isipokuwa wikendi hii ambayo alipakia picha wakiwa na Dk Choppa.