Otile Brown apokea zawadi kutoka YouTube baada ya kufikisha wafuasi milioni.

Muhtasari

• Msanii wa ngoma za kizazi kipya Otile brown amepokezwa kibao cha kumbukumbu na kampuni ya YouTube kama njia moja ya kumsherehekea kwa juhudi zake za kufikisha wafuasi milioni moja kwenye mtandao huo.

• Ushindi huu unakuja siku chache tu baada ya kuweka wazi kwamba wameachana na mpenzi wake wa muda mrefu kutoka Ethiopia, Nabayet.

Otile Brown
Image: Instagram

Msanii wa ngoma za kizazi kipya Otile brown amepokezwa kibao cha kumbukumbu na kampuni ya YouTube kama njia moja ya kumsherehekea kwa juhudi zake za kufikisha wafuasi milioni moja kwenye mtandao huo.

Baada ya tuzo hiyo, Otile Brown amekuwa msanii wa kwanza kutoka nchini Kenya kuwahi kufikisha idadi hiyo kubwa ya wafuasi katika mtandao wa YouTube.

Akisherehekea ushindi huo, Otile Brown amewashukuru wafuasi wake wote ndani na nje ya nchi kwa kumwezesha kutinga milioni moja na kuvunja rekondi ya wasanii wa humu nchini.

Otile Brown
Image: Instagram

“Angalia mlichokifanya wote mashabiki wangu. Nyinyi wote ni watu wa maana sana. Ahsante kwa ufuasi wa milioni moja kwenye mtandao wa YouTube,” aliandika Otile Brown kwenye Instagram yake.

Ushindi huu unakuja siku chache tu baada ya kuweka wazi kwamba wameachana na mpenzi wake wa muda mrefu kutoka Ethiopia, Nabayet.

Kufuatia ushindi huu, watu mashuhuri na mashabiki wake mbalimbali wameingia katika mitandao na kumsifia kwa jitihada zake hadi kufikia rekodi hiyo kubwa ambao haijapata kutokea kwa msanii yeyote nchini Kenya kabla yake.