Wanamitandao waitaka GAP kuvunja mikataba na Kanye West

Muhtasari

• Ukurasa Wa Gap (Instagram) Umejawa Na Maoni Ya Walimwengu Wakitaka Waache Kushirikiana Na Kanye West.

• Wengi Wamedai Kuwa Ni Kufuatia Vitendo Vyake/ Drama Anazozileta Katika Mtandao Wa Instagram Pamoja na Kumuitwa Mchekeshaji  Trevoh Noah Ni Mbaguzi.

Rappa Kanye West afungiwa Instagram
Rappa Kanye West afungiwa Instagram
Image: TMZ TV (Instagram)

Maji yanazidi kumfika msanii Kanye West Shingoni huku kampuni mbalimbali zikishinikizwa kuvunja mikataba ya ushirikiano na yeye kwa mabadiliko ya tabia yake.

Ukurasa wa kampuni ya GAP wa Instagram umefurika na watumizi wa mtandao huo ambao wengi wanaacvhia maoni wakiitaka ivunje mikataba ya ushirikiano na staa wa hiphop Kanye West kwa drama zake kwenye mtandao huo.

Kampuni hiyo ambayo inajihusisha na kutengeneza nguo na ambayo ina mkataba wa ushirikiano wa kibiashara na Kanye West, imewekwa chini ya shinikizo na wanamitandao ambao wanasema vitimbi vya West mitandaoni vimezidi na ni bora wajitoe katika maelewano naye ili kulinda heshima ya kampuni yao.

Haya yanakuja siku moja tu baada ya madai kuibuka kwamba Kanye West alimdhalilisha mchekeshaji wa mtangazaji kutoka Afrika Kusini Trevoh Noah kwa kutumia maneno ya ubaguzi wa rangi ya ngozi dhidi yake.

Instagram yenyewe ilichukua hatua ya kumpiga marufuku ya saa 24 ya kutotumia mtandao wa Instagram huku uchunguzi wa kina ukiendelea dhidi yake.

Msanii Kanye West anaendelea kuonesha tabia tofauti kabisa na awali kabla ya talaka huku wengi wakihisi huenda kuvunjika kwa ndoa yake na mwanamitindo Kim Kardashian kumepelekea tabia yake kubadilika ghafla.