Mtu wa mwisho kunikaribia sasa hivi ananyonyesha, Samidoh amuonya mwanadada

Muhtasari

• Usituletee temptation kwa hii kazi, na mimi nime-take after babu yangu. Mwenye alinikaribia hivo mara ya mwisho sasa hivi ananyonyesha - Samidoh alimwambia mwanadada huyo.

Kumeibuka video ya polisi na mwanamuziki wa Mugithi, Samidoh akijigamba kwamba yeye katika suala la kutopoteza nafasi katika kutunga mimba pindi inapojipa ni kama mila ambayo amerithi kutoka kwa babu yake.

Kwenye video hiyo, Samidoh anaonekana akimuonya vikali mwanadada ambaye alikuwa akicheza densi kwa kutingika mwili mzima mbele yake katika sehemu moja ya kujiburudisha alikokuwa akiwapiga tamasha la sherehe kwa mashabiki wake.

Samidoh alimwambia mwanadada huyo kwamba mtindo huo wa kucheza ni kama alikuwa anamletea majaribu na pia akasema mwenye alijaribu kufanya hivo mbele yake mara ya mwisho kwa sasa ni mama na ananyonyesha.

“Usituletee temptation kwa hii kazi, na mimi nime-take after babu yangu. Huwa siji na namba nzuri. Mwenye alinikaribia hivo mara ya mwisho sasa hivi ananyonyesha. Unaeza kaa kaa hapa ujipate Pumwani (hopitali ya kujifungua kina mama), sasa badala ya hiyo maneno, wee enda tu na uende kabisa lakini kama unataka, ubaki,” Samidoh anaonekana akimuonya mwanamke huyo.

Kwa kauli kwamba “mwenye alinikaribia hivo mara ya mwisho saai ananyonyesha,” wengi waliitafsiri kama msanii huyo amedokeza kuwa baba wa mtoto wa mwanasiasa Karen Nyamu ambaye wengi tu walikuwa wanajua wawili hao wako katika mahusiano ya kimapenzi na hata kuwa na mtoto pamoja.

Miezi michache iliyopita wawili hao walitupiana maneno kwenye mitandao ya kijamii kwa njia ya kuzuga ambapo Samidoh alikana kuwa baba wa mtoto aliyetarajiwa kuzaliwa, na Nyamu naye akajibu mipigo kwa kusema kwamba hajamshrutisha kukubali kuwa mtoto ni wake.