Karen Nyamu apendekeza Samidoh kumridhi Mzee Kibor kama mwenyekiti wa Men's Conference

Muhtasari

•Mgombea huyo wa useneti wa Nairobi amesema kuwa ucheshi na utata wa maisha ya Kibor zilifanya apendwe zaidi.

•Nyamu alimtaja baba ya watoto wake wawili Samuel Muchoki almaarufu Samidoh, ishara kuwa ndiye chaguo lake la mridhi wa Kibor.

Samidoh na Karen Nyamu
Samidoh na Karen Nyamu
Image: INSTAGRAM

Mwanasiasa na wakili mashuhuri Karen Nyamu amemwomboleza Mzee Jackson Kibor ambaye alifariki Jumatano usiku.

Katika ujumbe wake wa rambirambi ambao alichapisha Facebook, Nyamu amemtaja marehemu kama Jenerali wa mtoto wa kiume.

Mgombea huyo wa useneti wa Nairobi amesema kuwa ucheshi na utata wa maisha ya Kibor zilifanya apendwe zaidi.

"Mwenyekiti wa kongamano la wanaume Bw Jackson Kibor hayupo tena. Nimepokea kwa masikitiko makubwa taarifa za kifo chake. Yeye ni mtu ambaye sisi sote tulimpenda kwa ucheshi wake na mtindo wake wa maisha wa kuvutia. Nenda vizuri Jenerali wa Boy-Child. Pumzika kwa amani," Nyamu aliandika.

Mama huyo wa watoto watatu aliendelea kuuliza wafuasi wake wangependa nani aridhi wadhfa wa mwenyekiti wa kongamano la wanaume ambao marehemu Kibor ameacha nyuma.

Nyamu alimtaja baba ya watoto wake wawili Samuel Muchoki almaarufu Samidoh, ishara kuwa ndiye chaguo lake la mridhi wa Kibor.

"Sasa mnaona hio nafasi mzae amewacha vacant tupatie nani? Sijataja Samidoh," Nyamu alisema.

Kibor alifariki usiku wa kuamkia Alhamisi katika hospitali ya St Luke, mjini Eldoret baada ya kuugua kwa muda. Alifariki akiwa na miaka 89.