"Bado niko kwenye furaha ya kuwa mama mpya," Karen Nyamu azungumza baada ya kujifungua

Muhtasari

•Nyamu amesema kuwa kwa sasa amechukua muda wa mapumziko kutoka kwa kampeni ili kuunda uhusiano wa karibu na mtoto wake  ambaye alizaliwa Jumamosi.

Image: INSTAGRAM// KAREN NYAMU

Wakili na mwanasiasa mashuhuri Karen Nyamu ameweka wazi kwamba anafurahia hali yake mpya ya kuwa mama.

Akizungumza kupitia ukurasa wake wa Instagram, Nyamu amesema kuwa kwa sasa amechukua muda wa mapumziko kutoka kwa kampeni ili kuunda uhusiano wa karibu na mtoto wake  ambaye alizaliwa Jumamosi.

Ingawa bado hajaonyesha picha ya binti yake hadharani, Nyamu amedai kuwa mtoto huyo wake wa tatu ni mrembo kupindukia.

"Jamani yeye ni mrembo sana. Yeye ni mzuri sana, siwezi acha kumbusu. Nina raha, bado niko katika furaha ya mama mpya. Maisha yamepangwa," Nyamu amesema.

Mgombea huyo wa kiti cha useneta wa Nairobi katika uchaguzi wa Agosti ameweka wazi kuwa licha ya kuwa amejitenga na kampeni kwa sasa, timu yake ingali inaendelea kumpigia debe vizuri.

"Niko na timu nzuri, imetumwa kutoka mbinguni! Wanafanya kazi masaa yote wakati niko kwenye mapumziko madogo ya uzazi ili kuunda uhusiano na mtoto wangu," Nyamu amesema.

Mwanaiasa huyo alijifungua mtoto wake wa tatu siku ya Jumamosi na kumpatia jina Njeri. Mtoto huyo anaaminika kuwa wake wa pili na nyota wa Mugithi Samuel Muchoki almaarufu Samidoh.