Kumbe Diamond ni mhot, yeye ni crush wangu! - Murugi Munyi

Muhtasari

• Sikuwa najua kumbe he is hot, kumbe… anyway my new celebrity crush, Diamond - Murugi Munyi

Murugi Munyi, Diamond Platnumz
Murugi Munyi, Diamond Platnumz
Image: INSTAGRAM

Mwanablogu maarufu katika mtandao wa YouTube, Murugi Munyi ameibuka na mapya tena siku chache baada ya ku-trend katika mitandao ya kijamii kwa kukiri kufanya upasuaji wa kuondoa mafuta mwilini, kwa kimombo liposuction.

Munyi anakiri kuvutiwa ghafla na msanii kutoka Tanzania, Diamond Platnumz baada ya kumtazama katika kipindi cha uhalisia kwenye jukwaa la Netflix kwa jina Young Famous and African.

“Baada ya kutazama Young Famous and African, nimevutiwa ghafla na Diamond, sijui ni nini wadau lakini nimevutiwa sana na yeye. Ninahisi kwamba kabla nitazame kipindi kile kwenye Netflix, sikuwa najua mengi kumhusu kando na muziki wake na yale ambayo watu wanazungumza kumhusu. Lakini kipindi kile nimeona tu ukweli kabisa wa vile alivyo, kumsikiza akizungumza hata kama kizungu chake alikiboronga, haidhuru,” anaonekana akisema Munyi katika video ambazo alizipakia kwenye instastories zake.

Mwanablogu huyo pia amekiri kwamba sasa amepata picha kamili ni kwa nini kina dada wengi wanamzimikia mwanamuziki huyo.

“Sikuwa najua kumbe he is hot, kumbe… anyway my new celebrity crush, Diamond!” alisema kwa hitimisho.