Baba Levo atangaza kurudi shule, kumaliza masomo 2029

Muhtasari

• “Narudi shule, naamini sijachelewa. Nitamaliza chou 2029,” aliandika Baba Levo kwenye instastories zake.

Msanii Baba Levo
Msanii Baba Levo
Image: Instagram

Hivi umewahi jiuliza msanii mwenye utata ambaye pia ni chawa au kibaraka wa rekodi lebo ya Wasafi elimu yake ni ya kiwango kipi?

Basi kama ulikuwa unatilia shaka kiwango cha elimu yake utakuwa uko sahihi kabisa kwani msanii huyo ametangaza mwenyewe kwamba ndio mwanzo anarudi shule kuitafuta elimu.

Baba Levo anayejulikana na wengi kama mtu wa kububujikwa maneno mengi tu ambayo wengine wanayachukulia kama umbeya na wengine kusema ni kuzungumza bila kufikiria mara mbilimbili, anasema amefikia uamuzi wa kuifukuzia elimu sasa.

Msanii huyo aliandika kwenye instastories zake akisema kwamba anarudi darasani kuisaka elimu kwa udi na ambari, kibarua ambacho kitamgharimu zaidi ya miaka 7 ili kuimaliza na kupata ‘madigrii’

“Narudi shule, naamini sijachelewa. Nitamaliza chou 2029,” aliandika Baba Levo kwenye instastories zake.

Kwa kufikiria kwako unadhani Baba Levo atakuwa ameiachia elimu yake kiwango kipi labda?