'Mtasubiri' ya Diamond na Zuchu yavunja rekodi, views 100K chini ya dakika 37

Muhtasari

• Video hiyo ilipokelewa vizuri zaidi na kufikisha views zaidi ya laki moja chini ya dakika 37 tu tangua kupakiwa kwenye jukwaa la YouTube.

Zuchu na Diamond katika hali tete ya kimahaba
Zuchu na Diamond katika hali tete ya kimahaba
Image: Youtube screenshot

Itawachukuwa miaka zaidiya karne kwa sanii wengi tu haswa kutokea ukanda wa Afrika mashariki kuzipiku rekodi zinazoandikishwa na Staa wa bongo fleva Diamond Platnumz.

Usiku wa Jumanne, msanii huyo anayetamba kwa jina la kimajazi kama Simba aliachia video ya ngoma moja kutoka kwa EP yake ambayo aliiachia wiki kama mbili hivi zilizopita.

Video yenyewe ni ya ngoma Mtasubiri, ambapo amemshirikisha msanii mwenza kutoka Wasafi, Zuchu ambapo pia pamekuwa na tantarira nyingi tu mitandaoni kwamba wawili hao wapo katika penzi la siri.

Video hiyo ilipokelewa vizuri zaidi kwa njia ambayo haijawahi kutokea ambapo ilivunja na kuandikisha rekodi mpya ya ngoma katika ukanda huu kuwa na watazamaji yaani views zaidi ya laki moja chini ya dakika 37 tu tangua kupakiwa kwenye jukwaa la YouTube.

Baadhi ya wachanganuzi wa habari za burudani mitandaoni wanasema kwamba video hii imefanikiwa kutinga rekodi hizo baada ya maudhui yake kuonekana yakiwa yanaendana kwa ukaribu na matukio ambayo yamekuwa yakizunguka gumzo kuhusu uwezekano wa Diamond na Zuchu kuwa wapenzi kisiri.

Wengi wanasema collabo hiyo ni kama njia moja ya kuwachamba na kuwanyamazisha wale wanaosema kwamba penzi lao haliwezi kutokana na utofauti mkubwa baina ya wawili hao, ambapo wanaimba wakisema kwamba mambo kama hayo hayawahusu wenye midomo kaya na kama kusubiri basi watasubiri sana kungoja waachane.