'Jamani natamani kuolewa,' Wema Sepetu asema

Muhtasari
  • Walikuwa wamechumbiana kwa miaka miwili kutoka 2012 hadi 2014. Walikuwa na uhusiano wa karibu sana ambao uliwaongoza kufanya agano la damu
Wema Sepetu
Image: Wema Sepetu/INSTAGRAM

Kuwa na mpenzi maishani ni jambo zuri katika maisha ya kila mwanamume au mwanamke .

Kupata mtu wa kukuoa au kukuoa ni baraka. Inakuwa ngumu wakati watu wanazeeka lakini hakuna wa kumpenda au kumpa hisia zako kama mwanamke au mwanamume.

Muigizaji maarufu wa Tanzania wema sepetu anayefahamika kwa mafanikio yake kama miss Tanzanian 2006 amewashangaza mashabiki wake baada ya kusema kuwa anatamani kuolewa tatizo pekee ni kwamba hakuna mwanamume wa kumuoa.

"Jamani Natamani Kuolewa... Yaani nimetamani tu Harusi.... Na iwe Exquisite... The thought of me in a Wedding Dress, watu wamependeza... Food & Drinks na Good Music... Daaaaah...

Bibi Harusi nipo, Tatizo ni Bwana Harusi.... Bado hajajitokeza....🤔🤔🤔," Wema Aliandika.

Mrembo huyo yuko single na hajawa na mahusiano mazuri kama aliokuwa nayo na mwimbaji wa Tanzania Diamond Platnumz.

Kuachana kwao kulikuwa pigo kubwa baada ya hapo hawakuzungumza kwa miaka 3.

Walikuwa wamechumbiana kwa miaka miwili kutoka 2012 hadi 2014. Walikuwa na uhusiano wa karibu sana ambao uliwaongoza kufanya agano la damu.