Sababu ya akaunti ya Youtube ya Diamond platnumz kufungwa

Muhtasari
  • Sababu kwa nini akaunti ya Youtube ya Diamond platnumz imefungwa
Diamond Platnumz
Image: Hisani

Akaunti ya You Tube ya mwanamuziki maarufu kutoka Afrika Mashariki Diamond Platinumz imefungwa kwa kukiuka utaratibu na masharti ya mtandao huo.

Akaunti hiyo ilikuwa na wafuasi zaidi ya milioni 6 na video ambazo zimetazamwa na mamilioni ya watu.

Video yake maarufu aliyofanya na msanii kutoka Congo Dr Inno’s B ilikua na zaidi ya watazamaji milioni 100.

iKwa ujumla video zake zimetazamwa na watazamaji mara bilioni 1.

Sababu za kufungwa kwa mtandao zimeanishwa kuwa kukiuka masharti na sheria za mtandao.

Hatahivyo kwa mjibu wa meneja wa Diamond Hamisi Shaban Tale Tale amesema akaunt ya msanii huyo imechukuliwa na wadukuzi na hii ni mara ya pili kufanywa hivyo.