Wengi waliniambia nitoe vibao nilipokuwa naomboleza mume wangu-Ruth Matete Afichua

Muhtasari
  • Aidha msanii huyo amesema wakati wake wa kuomboleza Mungu alimpa nyimbo ambazo aliuwa anazirekodi kwa simu yake
ruthmatete
ruthmatete

Msanii wa nyimbo za injili Ruth Matete alivuma sana baada ya kumpoteza mumewe baada ya kulipukiwa na gesi nyumbani kwao.

Mengi yalisemwa wakati huo, huku msanii huyo akisalia kimya.

Mama huyo wa mtoto mmoja kupitia kwnye ukurasa wake wa instagram, amefichua kwamba kuna baadhi ya watu ambao walikuw na nia nzuri na wengine hawakuwa na nia nzuri huku wakimshauri atoe kibao wakati wa kumuombolea mumewe.

"Nilipokuwa nikiomboleza marehemu mume wangu Mchungaji BelovedJohn, baadhi ya watu waliniambia nirekodi wimbo au nyimbo wakati huo. Baadhi walikuwa na sababu za kweli na wengine hawakuwa nazo. Wengine walisema kuwa wimbo huo "utagonga" kwa sababu jina langu lilikuwa likivuma mitandaoni

Walakini, sikujiona tayari kurekodi wakati huo. Pia nilikuwa mjamzito sana na inaweza kuwa changamoto kutoa uwezavyo katika masuala ya uwezo wa sauti unapokuwa mjamzito.

Kwa hiyo nilisubiri. Hatimaye nilimlaza mume wangu. nilijifungua mtoto wa kike anayefahamika kwa jina @reynatoluwa na mambo yakaanza kuwa sawa taratibu."

Aidha msanii huyo amesema wakati wake wa kuomboleza Mungu alimpa nyimbo ambazo aliuwa anazirekodi kwa simu yake.

"Katika kipindi cha maombolezo yangu, Mungu alinipa nyimbo. Nilikuwa nikizirekodi tu kwenye simu yangu na kuzihifadhi.

Nina furaha kutangaza kwamba wakati ni sasa. Kusubiri kumekwisha. Nimesainiwa rasmi chini ya @stillaliveproduction!! Nina furaha sana! Ninafurahi sana kushiriki nyimbo ambazo Mungu alinipa pamoja nanyi!."