Huddah Monroe aomba kuunganishwa na mwanariadha Omanyala

Muhtasari
  • Huddah Monroe aomba kuunganishwa na mwanariadha Omanyala
Ferdinand Omanyala
Ferdinand Omanyala
Image: HISANI

Mwanasosholaiti maarufu nchini anaonekana kummezea mate mwanariadha Ferdinand Omanyala.

Huddah amekuwa akivuma mitandaoni kwa mambo tofauti,huku akionekana kuwakejeli wanaume wake Kenya, na kudai kwamba hawafahamu wala kujua kudekeza wapenzi wao.

Wiki jana kupitia kwenye ukurasa wake wa instagram alifichua tabia ya wauname mitandoni ambao wamekuwa wakimuomba pesa endapo ata wafuata kwenye kurasa zao za mitandao.

Pia alitoa sababu ya kutaka kuwa mwanamume kama kungekuwa na maisha ya pili.

Huddah aliendelea kuwaita wanaume walio na wahusika wa kuchekesha, kama wale wanaofikiri wanaweza kuzima kiu yao kwenye DM zake.

"Nikimfuata mwanamume kwenye mitandao ya kijamii kinachofuata ni DM,LOL mnakiu ata DM na kuomba pesa," alisema.

Kupitia kwenye ukurasa wake wa instagram mwanasosholaiti huyo alisema kwamba anataka kuunganishwa na mwanariadha ambaye ameibuka  hivi majuzi Omanyala.

"Omanyala sio mbaya vile Hapa kenya ni kama sitoki, unganisha hiyo date," Aliandika Huddah.