Bado mnaishi pamoja na ana mwanamke mwingine-Amber Ray amjibu Amira na kumwaya mtama

Muhtasari
  • Hatimaye mwanasosholaiti maarufu Amber Ray amejitokeza waziwazi na kujibu madai ya Amira kwamba amekuwa akijilazimisha kwa wanawe

Hatimaye mwanasosholaiti maarufu Amber Ray amejitokeza waziwazi na kujibu madai ya Amira kwamba amekuwa akijilazimisha kwa wanawe.

Kupitia kwenye ukurasa wake Amira wa instagram alimshambulia Amber na kumwambia anapaswa kukaa mbali na wanawe kwani alimuachia mumewe Jimal.

Huku akijibu madai hayo, Amber alisema kwamba Amira anatafuta kiki, na wakati mwingine anapaswa kumpigia simu ili watafute kiki vyema.

Hata hiivyo Amber alidai kwamba Jimal na mkewe wanaishi pamoja, licha ya wanamitandao kufahamu kwamba wametengana.

Alizidisha na kudai kwamba Jimal ana mwanamke mwingine kando na Amira.

"Jinsi watu wana tamaa ya kuwa maarufu inafanya niwe mgonjwa,yaani kwa mtu kuwa maarufu hii kenya ni lazima ataje jina langu,sio wazimu,sio walaghai na wengine nilitaka kupiga picha na watoto wake kwanini na kwa ajili na nani

Nimeshtuka watoto wako wanaweza danganya kiasi hicho lakini wana damu yako,ati uliniwachia Jimal utaacha lini kudanganya ulimwengu, nyinyi wawili bado mnaishi kwa nyumba moja, na anamwamke mwingine upande huo mwingine na uko sawa na hilo."

Aliongeza;

"Aki pesa wewe ooh ndoa tumetoka mbali, lakini ukweli ni kuwa nilikuachia Jimal lakini bado hungeweza kuwa naye, mwisho ukitaka kuwa maarufu wakati mwingine nipigie simu najua bado una namba yangu na kama huna mwambie mumeo akupe."