Kama nikuwekwa wacha niendelee kuwekwa-Guardian Angel ajibu madai ya kuwekwa na bibi yake

Muhtasari
  • Msanii wa nyimbo za injili nchini Kenya Guardian Angel amejibu madai kuwa anamtegemea mkewe Esther Musila
Image: INSTAGRAM// GUARDIAN ANGEL

Msanii wa nyimbo za injili nchini Kenya Guardian Angel amejibu madai kuwa anamtegemea mkewe Esther Musila.

Akiongea wakati wa mahojiano siku ya Ijumaa na Radiojambo, Guardian aliwaambia wakosoaji wake, akisema kwamba anajitegemea kikamilifu na anashughulikia bili zake zote bila msaada wa Musila.

Alikumbatia zaidi uvumi huo alibainisha kwamba angestahiki kumtegemea mke wake na wakosoaji wanapaswa kuachana na mambo yao ya ndoa.

"Kama hivi ndo kuwekwa acha niwekwe milele wacha niwekwe zaidi,Because kama nimewekwa hata sifai kupost anything ya the lady I'm purported to be with. I have never said that she is my sugar mummy secondly, I have never lived in her house, it is her who came to my house. Hajawai lipa any bills kwa nyumba yangu mimi ndo najilipia. Na kama mtu anahisi hio ndo kuwekwa basi iko tu sawa. Si mimi ndo nawekwa, wewe unawashiwa nini."

Kwa upande wake, Musila alisema tangu kufunga pingu za maisha na Angel, wamekuwa wakikejeliwa kwenye mitandao ya kijamii kwa madai ya uongo na haizuii familia yake.

"Nashangaa watu wanafikiria nini na jambo ni kwamba wanakuja na kila aina ya vitu bila kujua ukweli. Mimi husema   hao ni watu wasio na kazi, wajibambe mimi ninafurahia maisha yangu," alisema.