(+video)Wanaume huenda wakalazimika kutumia hela zaidi kusuka wapenzi wao kwa staili mpya

Kwa sababu ya kawaida ya wanawake kupenda mitindo mpya wa kusuka, wanaume huenda wakagharamia zaidi

Muhtasari

•Watumiaji wa mitandao ya kijamii wamekuwa na hisia tofauti baada ya video kusambaa kwenye mitandao ya kijamii ya mwanamke akitengeneza nywele zake

•Video hiyo ilionyesha mwanamke huyo akisongwa nywele zake katika staili  tofauti ili kuunda mtindo tofauti wa nywele shupavu. 

Linapokuja kwa  suala la mitindo na fasheni, watu huwa na njia tofauti za kujieleza na kuonyesha mitindo yao.

Hivi ndivyo hali ilivyo kwa mwanamke kutoka Nigeria ambaye staili yake ya nywele imeibua cheche  kwenye mitandao ya kijamii, na kuitwa majina mengi ya utani.

Mwanamke huyo alionekana kwa video iliyovuma kwenye mitandao ya kijamii  akibadilisha staili yake ya kusuka nywele zake kuwa mtindo wa kipeke.

Katika video hiyo, wanawake watatu wanaonekana wakitwist nywele zake na kuwa  nyuzi kadhaa.

Hata hivyo, mtindo huo wa nywele haukuwavutia watu wengi  wa mitandao ya kijamii haswa wanawake.

''Kuna mitindo mingi za nywele mbona angeweza kusonga kitu kizuri kwa kichwa'' mmoja kwa jina Bie.ola alisema.

"Mimi nilidhani kuwa baada ya kusogwa  staili hiyo ingekuwa wa kupendeza kichwani'' mwingine kwa jina  Clever_jhen alisema.

Kinyume na wengine kuna wanawake ambao walikuwa na mtazamo tofauti kuhusu staili hiyo.

''Kila mtu yuko huru kuweka chochote kile kwa kichwa chake, na si lazima kipendwe na kila mtu,'' Biem.bem aliongeza.

Wengine pia walimhurumia kwa yale machungu aliyapitia wakati alikuwa akisongwa.

''Kukaa chini hizo masaa zote ukisongwa si rahisi, najua  machungu huyu mwanamke aliyapitia wakati hizi shughuli zote kwa kichwa chake kilikuwa kikiendelea,'' Wendykoko alisema.

Kwasababu ya kawaida ya wanawake kupenda mitindo mipya ya kudamshi, wanaume huenda wakagharamia zaidi kwa njia ya kifedha ili kushughulikia wapenzi wao watakaopendezwa na hii mtindo ya nywele na kuisonga.