Mjenga Misuli alifariki kwa kujidunga sindano ya kuongeza misuli ya mikono hadi inchi 23

Segato, ambaye anatokea Sao Paulo, awali alisema alichochewa na umbo la mcheza filamu wa zamani Arnold Schwarzenegger

Muhtasari

• Alifariki akiwa na umri wa miaka 55 katika siku ambayo ilisemekana ndio alikuwa anajiandaa kusherehekea siku yake ya kuzaliwa huko Brazil.

Njebga misuli na muinua vyuma kutoka Brazil aliyefariki Valdir Segato
Njebga misuli na muinua vyuma kutoka Brazil aliyefariki Valdir Segato
Image: YouTube//screengrab

Mjenga misuli kutoka Brazili kwa jina Valdir Segato alitajwa kufa siku chache zilizopita kutokana na kujidunga sindano yenye  vitu ambavyo vilisemekana kuwa chanzo cha mauti yake.

Mjenga misuli huyo alipata umaarufu wa ghafla katika mtandao wa Tiktok baada ya kujidunga sindano ya mafuta ya kutishia maisha yake, mafuta ambayo ghafla yaliifurisha isuli yake ya mikononi kwa inchi 23.

Alifariki akiwa na umri wa miaka 55 katika siku ambayo ilisemekana ndio alikuwa anajiandaa kusherehekea siku yake ya kuzaliwa huko Brazil.

Vyanzo vya habari za kimataifa viliarifu kwamba Valdir Segato amekuwa akitumia sindano za synthol kwa miaka licha ya kuhatarisha kupata kiharusi na maambukizo ili kutengeneza misuli ya mikononi, kifuani, na mgongoni.

Segato, ambaye anatokea Sao Paulo, awali alisema alichochewa na umbo la mcheza filamu wa zamani Arnold Schwarzenegger na wahusika wa kubuni kama The Hulk, na alizungumzia jinsi alivyokuwa na fahari kujulikana mitaani kama 'mnyama mkubwa'.

Miaka sita iliyopita alionywa kwamba alikabiliwa na kukatwa mguu, au angalau uharibifu wa mishipa na ulemavu wa misuli, ikiwa angeendelea kutumia sindano ili kuzidi kunenepa kwa wingi. Lakini Segato, ambaye hapo awali alikuwa mfanyakazi wa ujenzi, alisema alipenda ufuatiliaji mkubwa wa Tiktok ulioletwa na umbo lake na alitaka kuwa mkubwa zaidi.

Kwa kujigamba alichapisha picha na video kwenye mitandao ya kijamii, akijiita 'Valdir Synthol' kwenye Instagram.

Lakini kulingana na vyombo vya habari vya nchini Brazil, kufikia wakati wa kifo chake alikuwa na marafiki wachache wa wageni, na aliishi maisha ya kujitenga licha ya ufuasi mkubwa kwenye mitandao ya kijamii kufuatia kupakia video zake kwa miaka mingi.